The House of Favourite Newspapers

VIDEO: ROMA Mkatoliki Kutekwa na Kupelekwa Kusikojulikana, Mkewe Afunguka Mazito

Kufuatia tukio la Rapa ROMA Mkatoliki kuvamiwa studio za Tongwe Records akiwa na wenzake kisha kupelekwa kusikojulikana, Global TV Online imefanya juhudi za kumtafuta mke wa Rapa Huyo, Mama Ivan ambaye amefunguka mengi kuhusiana na tukio hilo.

Taarifa za kukamatwa kwa ROMA zilianza kusambaa mapema jana usiku baada ya Mbunge wa Mikumi na Rapa Prof. Jay kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa ROMA na wenzake wamevamiwa na kukamatwa majira ya saa 1 usiku.

Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030, MONY @moni_ centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana..
Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!! Ameandika Prof. Jay.

Kutekwa kwa ROMA kumezua taharuki kwa familia ya Rapa huyo, wadau wa Bongo Fleva na Watanzania kwa ujumla.

Hii ni kauli ya mke wa ROMA, Mama Ivan

Comments are closed.