The House of Favourite Newspapers

Kuelekea Pasaka… Mnada wa Ng’ombe Pugu Wafurika


IKIWA imebaki wiki moja kufikia Sikukuu ya kuadhimisha kifo na ufufuko wa Yesu Kristo ‘Pasaka’, baadhi ya wananchi wameonekana kufurika katika Mnada wa Ng’ombe uliopo Pugu jijini Dar es Salaam.

Kamera ya Global Publishers imefanikiwa kunasa baadhi ya matukio yanayoonesha wananchi na wauzaji wa mifugo yao wakiwa katika mnada huo,ambapo wengi wao wanajiandaa na kununua mifugo inayouzwa katika mnada huo kwa ajili ya kitoweo kwenye sikukuu hiyo.

Nimekuwekea picha 6 ushuhudie wananchi walivyofurika mnadani leo.

Picha: Denis Mtima

Comments are closed.