The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Bomoabomoa Mpanda ni Vilio Tupu, Mamia ya Nyumba Zabomolewa

0
Bomoabomoa.

Bomoabomoa Mpanda ni Vilio Tupu, Mamia ya Nyumba Zabomolewa Wakazi wa maeneo ya Tambukareli, Mpanda Hotel na Msasani, wamejikuta katika sintofahamu baada ya Shirika la reli Mkoa wa Katavi kuwataka kubomoa nyumba zao baada ya kuvamia reli na mali zake.

Zoezi hilo ambalo limezikumba kaya takribani 200 kufuatia agizo hilo ambalo wakazi hao wamesema kuwa wao wanashangazwa vipimo vilivyotumika na shirika hilo.

Global TV ikizungumza na wakazi hao, wamedai kuwa wao wapo maeneo hayo toka mwaka 1974, jambo ambalo linawashangaza ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Lilian Matinga kuwataka kubomoa wao wenyewe nyumba zao na mpaka ifikapo Januari, 2018 wawe wameondoka.

 

Global TV ilifika ofisini kwake mkuu huyo wa wilaya ili kupata ufanunuzi wa mgogoro huo lakini mwandishi wa habari hii aliambiwa mkuu yupo kwenye ziara ya kikazi hata alipopigiwa simu kwa muda wa wiki moja bado hakupatikana hewani.

Hata hivyo, Global TV iliendelea kumtafuta mkuu huyo wa wilaya na kumpata akiwa katika kikao cha baraza la madiwani lakini alivyotakiwa kutoa ufafanuzi akaishia kumuuliza swali mwandishi wa habari hii reli imejengwa mwaka gani.

 

Bomoabomoa Mpanda ni Vilio Tupu, Mamia ya Nyumba Zabomolewa

Leave A Reply