The House of Favourite Newspapers

Video: Dkt Mpango Aongoza Maadhimisho ya Siku ya Mazingira

0

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amewataka wafanyabiashara hasa wa gesi ya kupikia majumbani kubuni mbinu za kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini ili waweze kumudu gharama za nishati hiyo mbadala.

 

Hiyo ni kutokana na kile kilichobainishwa kuwa Watanzania wengi bado wanatumia mkaa na kuni kama vyanzo vya kupikia jambo ambalo linachangia uharibifu wa misitu.

 

Ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 5, 2021 katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma yenye kauli mbiu ya “Tutumie Nishati Mbadala Kuokoa Mfumo wa Ikolojia”.  Amesema licha ya uwepo wa baadhi ya nishati mbadala ambazo watu huweza kuzitumia kama vyanzo vya kupikia lakini ukuaji wa matumizi wa nishati hizo ni wa asilimia mbili tu kwa mwaka.

 

“Tatizo kubwa lililo mbele yetu ni namna gani unapunguza bei ya nishati mbadala na bei ya majiko, sasa naomba niwasihi vyuo vyetu na vinginevyo, watafiti ni nini kinasababisha bei ya nishati mbadala na vifaa husika kuwa kubwa na nini kifanyike.”

 

“Kama ni kuangalia mfumo wa kozi basi tuutazame lakini pia kama ni gharama za kuzalisha nishati mbadala nazo ziweze kutazamwa,” amesema

 

Amesema Serikali, wadau wa maendeleo na asasi za kiraia na sekta binafsi hazina budi kuelekeza nguvu zaidi katika kutekeleza miradi inayolenga kuongeza matumizi ya nishati mbadala ya kupikia ikiwemo gesi, matumizi ya umeme wa jua, matumizi ya majiko banifu na vifaa vinavyotumia nishati kidogo katika kupika.

Leave A Reply