The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Washindi wa Spoti Hausi Smart Phone Walivyopatikana Zawadi Zao

0

HATIMAYE washindi wawili wa Shindano la Spoti Housi Smart Phone, wamepatikana leo, katika mchakato wa kuchuja majina uliofanyika mubashara kupitia Global TV Online ambapo wamejipatia simu kali za kisasa, aina ya Tecno WX3.

Wahindi hao ni Joseph Kimagula mkazi wa Iringa Mjini ambaye anatumia jina la Mkata Kiu TV na Chaz Muro ambao walipigiwa simu moja kwa moja na kuulizwa maswali machache yaliyothibitisha uhalali wa ushindi wao na kisha kupewa maelekezo ya namna ya kuzipata zawadi zao.
Kipindi cha Spoti Hausi huruka kila siku ya Alhamisi, kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na moja kamili jioni. Kutazama kipindi hiki, ingie YouTube na kisha andika Global TV Online na hapo utapata fursa ya kutazama kipindi hiki bora kabisa cha michezo, kikiendeshwa na wachambuzi mahiri na wabobezi wa masuala ya michezo na burudani, wakiongozwa na Saleh Ally ‘Jembe’.

Leave A Reply