The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Hali Ilivyokuwa Bungeni Mtoto wa Ndesamburo Alivyopata Taarifa za Kifo cha Baba Yake

0

BUNGENI, DODOMA: Hali ilibadilika ghafla Bungeni mjini Dodoma leo baada Mtoto wa Marehemu Mzee Philemon Ndesamburo, Lucy Owenya kupewa taarifa za msiba wa baba yake.

Mzee Philemon Ndesamburo, aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Chadema Arusha, Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro, ameafariki dunia baada ya kuzidiwa ghafla ofisini kwake kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Moshi.

Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe;

“Jana akiwa mzima alimpigia simu Meya wa Arusha Kalist Lazaro ili ampatie rambirambi ya milioni 3.5 kwa wahanga 35 wa ajali ya Lucky Vincent. Meya alifika ofisini kwa Ndesamburo majira ya saa 4 asubuhi.

“Wakati mzee alipochukua kalamu kuandika cheki kwa ajili rambirambi hiyo, alilegea, akadondosha kalamu, kutokana na hali hiyo Meya aliamua kuita wasaidizi ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa KCMC ambapo baada ya kufikishwa hospitalini hapo, nusu saa baadaye madaktari walisema ameaga dunia.” Alisema Mbowe.

 

Leave A Reply