The House of Favourite Newspapers

JPM Azindua Kanisa Dodoma, Achangisha Pesa za Kujenga Msikiti -( Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishiriki na waumini wengine katika Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” ambapo pia alizindua Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Rais Magufuli leo Agosti amehudhuria Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, Ibada ya Misa Takatifu inaongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya.

Baba Askofu Mkuu, Mhashamu Beatus Kinyaiya amewataka waumini kuzusha macho kuuona uzuri wa kanisa na kuwaasa uzuri wa kwanza ni roho hivyo waumini watamani roho zao zipendeze kama kanisa lao, Baba askofu mkuu amemkaribisha Rais Magufuli ili awamegee busara zake.

 

Rais Magufuli: Matokeo ya ujenzi wa kanisa hili umefanywa na wakristo wote, wakati wa ujenzi kila mmoja alitoa alichokuwa nacho. Nakumbuka katika siku hiyo mama mzee mmoja alitoa 5,000 yote aliyokuwa nayo katika ujenzi wa kanisa hili, ujenzi umefanywa na waumini wote wa kanisa hili.

Nawashukuru wananchi wengine mbalimbali siku hiyo tukitoa mchango hapa nilikuwa napigiwa simu na baadhi ya watu wengine waislamu nakumbuka nilipigiwa na mtu mmoja kutoka Dar es Salaam na akaja kukabidhi milioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hili, wadau ni wengi waliojitolea na mimi nawashukuru sana kwa niaba yenu.

 

Nawashukuru wasimamizi ambao fedha tulizozichanga hawakuzila na shetani alikimbia mbali kuhubiri roho zao kuzila fedha hizi, tunawashukuru wajenzi hawakupoteza muda chini ya uongozi wa mkuu wa JKT na vijana wake, walikuja na kushiriki katika ujenzi huu. Vijana walioshiriki ujenzi huu si wakristo tu, walikuwepo Waislamu wamejenga, Roman, Wasabato, KKKT, Anglingana na waliookoka wamejenga.

Kikosi cha JKT nilichokiomba tukawapa fedha zilizokuwa zimechangwa na ninyi na zimechangwa na wananchi wengi napenda kuwapongeza kwa niaba yenu kwa sababu wamefanya kazi nzuri sana na huu ndio umoja wa watanzania.

Mhasham baba Askofu mkuu ndio maana mimi nilisita sana kuambiwa mimi ndie mfadhili mkuu kwa sababu ninaamini waliofadhili kanisa hili na kushiriki kwa njia moja au nyingine kukamilisha. Nilisita kubeba heshima hiyo ambayo sistahili, mimi nilitoa mapendekezo nikachangia kidogo nilichokua nacho lakini kimechangiwa kingi na wale walioshiriki kwa hiyo pongezi ni kwetu sisi sote.

Nimefurahi kumuona father Kitima, huyu ni rafiki yangu wa siku nyingi. Alikuwa ndio vice chancellor wa St. Augustine, chuo kikuu cha kule Mwanza na baadae akateuliwa kuwa katibu mkuu wa baraza la maaskofu na leo nimefurahi kuja hapa. Yale mengine mengine maviporo viporo yanayobaki kule na kwa kuwa wewe ndie katibu mkuu wa maaskofu wote, hata hili la fence linaweza likakugusagusa kidogo. Ukaangalia angalia yale yanayobaki huko ili utusaidie sisi.

 

Parokia ya Chamwino ina raha yake, ina upendo mkubwa hata nyimbo mnaona zinavyogusa na uwepo wa Mungu upo, kwa ruhusa yako baba askofu ilikuwa niombe kitu kimoja. Kanisa hili wameshiriki watu wa madhehebu mbalimbali kulijenga na kiukweli mahali ambako ni makao makuu panatakiwa kuzungukwa na watu wanaomtukuza Mungu. Sio wa dhehebu moja bali yote kadri muda utavyokuwa unaenda, makao makuu lazima paende na uwepo wa Mungu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua msikiti wa Chamwino na maemneo yake baada ya kuendesha harambee ya kuchangia ujenzi wake wakati wa Misa Takatifu ya Dominika ya 21 ya Mwaka “A” wakati wa uzinduzi wa Kanisa, Nyumba ya Mapadres na Grotto ya Parokia ya Bikira Maria Imakulata Ikulu Chamwino leo Jumapili Agosti 23,. 2020

Kama utaniruhusu, tutumie siku ya leo pia tuchange angalau tuanze kujenga msikiti wa ndugu zetu waislamu ambao msikiti wao ni mdogo nao wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu na baadhi ya wasaidizi wangu wengine ni waislamu na nataka niwatajie mmoja tu, kuna Alhaji, ameshaenda kuhiji mpaka Makka lakini ni msaidizi wangu. Ninapoingia humu inabidi lazima aingie humu kanisani lakini inapofika siku ya kwenda kumtukuza Mola wake, nimeambiwa ule msikiti bado haujawa mkubwa vizuri.

 

Baba Askofu, uniruhusu leo nichukue kikapu ili kama sitachukua muda wako mwingi niwaombe wakristo wenzangu tuanze kuchangie, tutamuomba baba Paroko akaziwasilishe kwa shekhe kwenye msikiti wetu na tutajipanga taratibu namna tutakavyoweza kuukarabati.

 

Tukimaliza hivyo tutaendelea tena katika kanisa jingine kama ni Anglikana, KKKT, Wasabato ili utukufu wa Chamwino katika kumtukuza Mungu ukasimame.

Rais Magufuli amechukua kikapu na mtu wa kwanza kuchangia ni baba Askofu ambae ametoa laki mbili na msaidizi wake ambae ni Alhaji atachangia lakini tatu.

 

Katibu mkuu wa baraza la maaskofu nae kachangia laki moja na ameeleza amemfahamu Rais tangu mwaka 2001 na alikuwa karibu sana na maaskofu na amemfahamu kupitia kwao hata leo anachokifanya inaonyesha namna gani anawapenda watanzania na amefanya vingi vinavyofanya nchi iende mbele kama rushwa iliyokuwa inaelekea kutushida,a anasema ukipita kila mahali wanasema tupeni sisi Rais Magufuli.

Jumla ya fedha zilizochangwa ni 48,021,000/= Mifuko ya simenti 48 na lori tano za mchanga.


⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply