The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Hii ni Kauli ya Nay wa Mitego Baada ya Kuibuka Dodoma kwa Mwakyembe

HATIMAYE Rapper Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amewasili mjini  Dodoma na kufanikiwa kufanya mazungumzo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe kwa ajili ya kupewa maelekezo ya Rais Dkt. John Magufuli kuhusu wimbo mpya  wa rapa huyo ‘Wapo’ ambao mwanzoni ulidhaniwa kuwa una maneno ya kuikashfu serikali.

Akizungumza na Global TV Online, haya ni maneno ya Nay wa Mitego baada ya kumaliza kuzunumza na Mwakyembe.

“Nimekuja mpaka Dodoma, nimefanikiwa kuzungumza na Waziri Mwakyembe mambo mengi, kuanzia Jumatatu nitakuwa free kuzungumza yote kuhusu tuliyojadiri.

“Nawashukuru mashabiki wangu wote, nwapenda sana mashabiki wangu, waendelee kunisapoti.

” Hakuna kitu chochote kilichobalika, sijabadili mawazo kwenye kichwa changu, WAPO tuendelee kui-push ili ujumbe uendelee kufika, WAPO, WAPO, WAPO! Alisema Nay.

Nay alihamishiwa katika Kituo cha Kikuu cha Polisi (Sentro) jijini Dar es Salaam kutoka Mvomero, Morogoro alikokuwa anashikiliwa na polisi kuanzia asubuhi ya Jumapili, Machi 26 kutokana na kuachia wimbo unaodaiwa kuwa una maneno ya kichochezi na kuikashfu serikali iliyoko madarakani ambapo baadaye Rais Magufuli alitoa agizo kuwa msanii huyo aachiwe huru na wimbo wake uendelee kupigwa huku akitoa maelekezo kuhusu mambo kadhaa ambayo msanii huyo anapaswa kuyaongeza kwenye wimbo huo.

MSIKILIZE NAY WA MITEGO HAPA AKIFUNGUKA

Comments are closed.