The House of Favourite Newspapers

Video: Kiama cha wenye Vyeti feki, Watumishi Hewa Kimewadia! – Rais Magufuli

0


Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mabweni mapya UDSM.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa hafla hiyo.

Sehemu ya umati wa wananchi wakiwemo wanafunzi wa UDSM waliohudhuria kwenye hafla hiyo

Viongozi wakiimba wimbo wa Taifa.

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie waliohudhuria.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo ametangaza ‘kiama’ kwa kuhusu sakata la watumishi hewa pamoja na viongozi wa serikali ambao wamefoji vyeti.

Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako akihutubia.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua rasmi mabweni mapya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambayo yamejengwa na Jeshi la JKT kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo Nchini (TBA) huku yakigharimu kiasi cha Tsh. bilioni 10 hadi kukamilika.

Rais Magufuli akiwasili.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa, mabweni hayo yenye uwezo wa kubeba wanafunzi 3840, yataondoa adha ya malazi kwa wanafunzi wa chuo hicho ambao wengi wao walikuwa wakiishi mbali ya chuo hivyo kuwafanya wakoswe baadhi ya vipindi vya masomo huku akiagiza walipie Tsh. 500 kwa siku badala ya Tsh. 800 wanayolipa kwa sasa.

Rais pia ameitaka Tume ya Udahili ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo vya kwenda kusoma na badala yake wawachague wanafunzi hao kulingana na maombi yao.

…Wakienda kuzindua.

Baadhi ya kauli alizozizungumza Rais Magufuli leo ni hizi hapa.

Wataalam walisema mradi huu ungegharimu bil.150 mpaka bili.170 kukamilisha, ilikuwa ni lugha ya kukatisha tamaa. Tatizo la makazi liliwasumbua wanafunzi wengi UDSM. Kuna waliolazimika kuoa au kuolewa ili tu wapate makazi ya kuishi.

Wengi waliokuwa wakipanga vyumba mitaani, walipanga katika maeneo hatarishi huku wengine wakilala kwa zamu.

Baadhi ya wanakwaya wakiimba.

Nashukuru tuliweza kupata eneo la kujenga hapa, si kama Mabibo Hostels walivyoacha eneo hapa wakaenda kujenga huko mbali.

Nina matumaini makubwa vijana hawa watayapenda haya mabweni. Wanafunzi watalipia mabweni kwa gharama ya Tsh. 500 kwa siku badala ya Tsh. 800 kama ilivyo kwenye mabweni mengine UDSM.

Serikali ya awamu ya tano imejitoa kuwekeza katika elimu. Naagiza wanafunzi wawe wanachagua vyuo badala ya TCU kuwapangia chuo cha kwenda kusoma. Mtu anafaulu anataka aje asome Chuo Kikuu Dar es Salaam kwenye mabweni ya lakini anapelekwa kwenye chuo kingine

Watoto wawe na haki ya kuchagua vyuo wanavyovitaka. Vile ambavyo havitachaguliwa vife. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wanakipenda kwa sababu ya ubora wa elimu yake. Suala sio wingi wa vyuo vikuu nchini lakini ni ubora wa vyuo hivyo. Ni bora kuwa na vyuo vikuu vinne vyenye wanafunzi wa kutosha.

Mama Getrude Rwakatale akiwasili eneo la tukio.

Chuo Kikuu cha Mloganzila kitakapokamilika wanafunzi wa udakatari waliopo hapa UDSM wahame wapelekwe kule kwenye vifaa vingi.

Kwanini mabasi ya UDSM hayapo? Yangesaidia kuchukua wanafunzi wa mabibo badala ya kuwaacha kila siku wagombanie daladala.

Rais Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mabweni hayo.

Je! Walionunua mabasi yale mawazo yao hayakuwa mazuri? Kama yalikuwa mazuri, kwanini mmeshindwa kuyaendeleza?

Nilidhani Mbunge wa Ubungo leo angekuwa hapa aniombe chochote na mimi ningempatia. Mwambie alete shida zenu serikali itazitatua.

Siku nimemteua Prof. alikwenda kwa kusoma Ilani ya CCM katika kipengele kinachohusu sekta ya maji.

Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam itashangaa kama itakosa maji wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji alikuwa mhadhiri hapa.

Nilipoteua balozi wa Israel wengi walikosoa, lakini kwa kufanya hivyo tu, watalii wengi kutoka Israel wamekuja nchini kutalii.

Ninafahamu changamoto za walimu UDSM ni nyingi sana, ila nawaomba muendelee kuwafundisha hawa vijana, tutazifanyia kazi.

Baadi ya Mabweni hayo.

Ninasubiri ripoti ya watumishi wa serikali wenye vyeti feki ambao naambiwa wanafika 9,000 ili nianze kuifanyia kazi. Baadhi ya viongozi wa vyo mbalimbali wamekuwa wakienda TCU kuomba wapangiwewanafunzi kwenye vyo vyao.

HOTUBA YA RAIS MAGUFULI UZINDUZI WA MABWENI MAPYA UDSM

Leave A Reply