The House of Favourite Newspapers

Video: Kilichomuua Godzilla; Dada Asimulia: “Aliona Watu Wanamfuata”

KWA mujibu wa madaktari, kifo cha mwanamuziki Golden Jacob Mbunda ‘Godzilla’ kilitokana na mchanganyiko wa malaria, kupanda kwa kisukari na kushuka kwa presha.

 

Dada wa marehemu Godzilla aitwaye, Joyce Mbunda, amesema hivyo katika mahojiano aliyofanya na Global TV Online ambapo alisema matatizo yaliyopelekea kifo cha mwanamuziki huyo kijana yalianza Jumapili iliyopita alipokuwa anajisikia vibaya na kuanza kutapika, hali iliyosababisha ndugu wampeleke hospitali.

 

Akisimulia tukio hilo kwa masikitiko, Joyce alisema baada ya kumfikisha hospitali na kupimwa, daktari alisema tatizo lilikuwa ni malaria, kupanda kwa kisukari na kushuka kwa presha, hivyo alimpa dawa za kukabiliana na tatizo hilo na wakaruhusiwa kurudi nyumbani.

 

Hata hivyo, baada ya kurudi nyumbani, marehemu alizidi kutapika akidai kulikuwa kuna kitu kimemkwama tumboni na kwamba nguvu zilikuwa zinamwishia, hali ambayo iliwalazimu kumrudisha hospitali tena kwa ajili ya matibabu alikoendelea kupata matibabu hadi jana waliporudi nyumbani.

 

Akiwa nyumbani akiendelea kupata dawa chini ya uangalizi wao, aliingia chumbani kulala lakini, kwa mujibu wa Joyce, kaka yake alianza kusema aliona watu wanamfuata na hivyo kumwomba amfiche wasimfuate ambapo walibidi wamshike asizidi kuhangaika.

 

Ni wakati wakiwa wamemshika ndipo Godzilla — mmoja wa wanamuziki maarufu nchini katika midundo ya Bongo Flava — alikata roho usiku wa kuamkia leo na kufariki dunia.

Kuhusu maziko ya marehemu, Joyce amesema wanasubiri uamuzi wa familia yao.

TUMEKUWEKEA MAHOJIANO KAMILI KATI YA JOYCE NA GLOBAL TV ONLINE:

Tanzia: Msanii Godzilla Afariki Dunia

Comments are closed.