The House of Favourite Newspapers

VIDEO: RC MAKONDA AWAPA ULAJI WACHONGA VINYAGO NA WACHORAJI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisani kitabu cha wageni eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Agosti 3, 2019 ametangaza akiwa eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam kwenye maduka ya wachonga vinyago kuwa ifikapo Agosti 06 mwaka huu  atafunga barabara zinazozunguka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  zenye ukubwa wa Mita 700 ili eneo hilo litumiwe na wachonga vinyago, wachoraji wa picha na watengeneza shanga kuuza bidhaa wanazozalisha kwa
ndani ya siku 15 za ugeni wa viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) wanaotarajiwa kuingia Agosti 09, jijini Dar es Salaam.

RC Makonda amesema kwakuwa eneo hilo lipo jirani na Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere unapofanyika mkutano huo itakuwa rahisi kwa wageni kutembelea wafanyabiashara hao na kununua bidhaa mbalimbali zinazatengenezwa kwa umahiri na ubunifu mkubwa ikiwemo Vinyago, Picha za kuchora, Shanga na Vinyago jambo litakalosaidia pia kutangaza utalii wa Tanzania.

Aidha RC Makonda amesema eneo hilo pia litakuwa na ulinzi wa kutosha na litafungwa Taa za kisasa ili kuhakikisha wageni wafika na kununua bidhaa muda wowote kwa kipindi chote cha mkutano wa Jumuiya ya SADC jambo litakalosaidia kukuza uchumi wa wauzaji na Taifa kwa ujumla.

Hata hivyo RC Makonda amesema ni vyema Wananchi wakauchukulia Ugeni huu wa Viongozi zaidi ya 16 wa Jumuiya ya SADC kama sehemu ya fursa ya kuuza na kutangaza bidhaa zao.


Comments are closed.