The House of Favourite Newspapers

Kigogo Wizara ya Fedha Aliyejinyonga Azikwa Karagwe

MWILI wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango, Leopold Lwajabe,  umezikwa leo Jumamosi Agosti 3, 2019,  katika kijiji cha Ihembe wilayani Karagwe Mkoa wa Kagera.

Ibada ya mazishi iliongozwa na Paroko wa Parokia ya Nyaishozi Jimbo Katoliki Kayanga, Padri Vitalis Bamuhiga, aliyewataka  ndugu wa marehemu na mamia ya wananchi  walioshiriki ibada hiyo kumkabidhi Mungu maisha yao duniani.

Amesema kuna maswali magumu ambayo mwanadamu hana majibu na kwamba kifo cha Lwajabe kimeacha maswali ambayo hakuna mwenye majibu.

Lwajabe aliyekuwa mkurugenzi wa miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini (EU) kupitia wizara hiyo, mwili wake ulikutwa wilayani Mkuranga mkoani Pwani Julai 26, 2019 akiwa amejinyonga, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

 

 

Comments are closed.