The House of Favourite Newspapers

Video ya Utupu Yamkwamisha Nandy Kupanda Daladala

Faustina Charles ‘Nandy’

MKALI wa Ngoma ya Ninogeshe, Faustina Charles ‘Nandy’, amesema kuwa anatamani sana apande daladala ili akutane na mashabiki wake uso kwa uso ila dhamira hiyo ilikatishwa na video yake ya faragha na mwanamuziki mwenziye, William Lyimo ‘Bill Nas’ iliyovuja kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza Showbiz Xtra Nandy alisema kuwa, alipanga karibu mwezi mzima kufanya ziara hiyo ya kila sehemu atakayoenda atumie usafiri wa daladala ili aweze kupata nafasi nzuri ya kujua mambo mbalimbali ndani ya daladala na kuna wakati anazitamani stori za humo.

“Nilipanga ndani ya mwezi mzima usafiri wangu uwe huo lakini mambo yakaingiliana na ya kusambaa ile video ya faragha kwenye mitandao ya kijamii, lakini bado dhamira yangu ipo nitafanya hivyo kwa sababu natamani kukutana na watu tofauti

IMELDA MTEMA

Comments are closed.