The House of Favourite Newspapers

Vifo vya Mama Wajawazito sasa Basi Kata ya Luharanyonga Buchosa

0

Kutokana na kutokea kifo cha mama mjamzito miaka kadhaa iliyopita kilichosababishwa na ukosefu wa huduma ya afya katika Kijiji cha Iseng’he Kata ya luharanyonga Halmashauri ya buchosa wilayani Sengerema, Serikali imetoa zaidi ya Sh152milioni kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati iliyoanzishwa na nguvu za wananchi na ujenzi wa nyumba ya mganga kwenye Kijiji hicho.

Tukio la mama mjamzito Maritha Maingu kupoteza maisha wakati akiwahishwa kwenye Kijiji jirani cha Luharanyonga umbali wa kilometa saba kwa ajili ya kujifungua.

Mume wa Marehemu huyo Musa Daudi amesema kifo cha mke wake Maritha Maingu wakati wa kujifungua kilisababishwa na kukoswa kwa huduma za afya kwenye Kijiji hicho kitu ambacho kilifanya wananchi waamue kuanza ujenzi wa zahanati ili kunusuru maisha ya wakinamama wengine.

” Mke wangu alikosa huduma ya afya kutokana na kijiji chetu kukosa Zahanati na huduma kuwa mbali kama ingekuwa karibu kifo cha mke wangu kisinge tokea ameniachia watoto watano nawalea mwenyewe lakini angekuwepo tungeshirikiana kuwalea”amesema Musa.

Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Iseng’he Daud Serengeti amesema baada tukio hilo wananchi walianza kujitolea nguvu kazi zao kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ambayo itawasaidia kupata huduma za afya.

Kijiji hicho ni miongoni mwa vijiji vitatu vinavyounda Kata ya Luharanyonga ambacho kina wakazi wapatao 4700 huku Kijiji hicho tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975 hakijawahi kuwa Zahanati.

Mbunge wa Buchosa Eric Shigongo amewatoa hofu wananchi wa Kijiji cha Iseng’he kuwa Serikali imeweka mpango mkakati wa kuhakikisha Zahanati hiyo inakamilika na kufunguliwa ili kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Kijiji cha Iseng’he.

Ambapo hadi sasa fedha zaidi ya Sh152 zimetolea kukamisha zanahati hiyo sambamba na kujenzi wa nyumba ya mganga wa Zahanati hiyo ambapo Sh50milioni zimekamalisha ujenzi wa Zahanati na Sh102milioni zinajenga nyumba ya mganga.

Kwa upande wake diwani wa Kata ya Luharanyonga Hezeron Samike amemshukuru mbunge wa Buchosa Eric Shigongo kwa kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo ambazo zitasaidia kumaliza changamoto hiyo Kwa wananchi wa Kijiji cha Iseng’he kupata Zahanati.

Leave A Reply