The House of Favourite Newspapers

Vigogo wa Jeshi la Polisi Wakamatwa na Magari Matatu ya Wizi

kamanda-mutafungwaWakazi wa Mji mdogo wa Himo wilayani Moshi wameshangazwa na kitendo cha Jeshi la Polisi mkoani humo kutowachukulia hatua maofisa wake wawili wanaohusishwa na mtandao wa wizi wa magari.

Maofisa hao wawili wanaotuhumiwa, mmoja anacheo cha Mrakibu wa Polisi (ASP) na mwingine Koplo walikamatwa na magari matatu ambayo waliyasafirisha hadi jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya Polisi zinaeleza kuwa maofisa hao walikamatwa na kikosi kazi maalum kutoka Dar es Salaam tangu mwezi uliopita lakini hadi leo hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

Katika operesheni hiyo, mtuhumiwa mwingine ambaye ni raia alikamatwa nyumbani kwa Koplo huyo akiwa na gari moja la wizi na vibao vya namba za magari 70.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa alipoulizwa na gazeti la Mwananchi alikiri maofisa hao kukamatwa na magari hayo akasema lakini mtu hawezi kupewa adhabu kabla ya kuthibitika kuwa kafanya uhalifu.

Comments are closed.