The House of Favourite Newspapers

Vijana waandaa mbio za magari kupinga ujangili

0

1Mkurugenzi wa Mawasiliano wa (BRCC), Krantz Mwantepele, akifafanua jambo katika mkutano huo. Kulia ni mratibu wa tamasha hilo, Idrisa Magesa.

3Idrisa Magesa akifafanua jambo.
4Mkutano ukiendelea.

2Wanahabari wakiwa kazini.

KUNDI la vijana linaloojiita Bongo Ride Charity Cruise (BRCC) limeandaa tamasha la mbio za magari ambalo litaanza kutimua vumbi jijini Dar, Machi 25 kuelekea mkoani Arusha ambapo linatarajiwa kuhitimishwa Machi 27 mwaka huu hukohuko mkoani Arusha.

Mbio hizo zitatimua vumbi katika viunga mbalimbali vya mkoani Arusha na kuelekea katika hifadhi ya Tarangire mkoani humo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, mratibu wa tamasha hilo, Idrisa Magesa, alisema wakiwa mkoani Arusha watazungumza na watu mbalimbali wakiwemo wakazi wa mji huo na kuwaelimisha umuhimu na thamani ya wanyamapori kama tembo na wengineo.

(PICHA : RICHARD BUKOS / GPL)

Leave A Reply