The House of Favourite Newspapers

Wawili Wakamatwa na Dawa za Kulevya

0
 Kaimu Kamishna Jenerali wa  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Wilbert Kaji (kushoto) akiwaonyesha watuhumiwa wawili, Stanley Salvatory Ngowi au Sultan Salvatory Ngowi na  Jimmy Walter Mlaki, waliokamatwa wakidaiwa kusafirisha madawa ya kulevya. 

MAMLAKA  ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imeendelea na kasi yake ya kuumaliza mtandao wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya kwa kuwakamata vijana wawili waliokuwa wakisafirisha dawa hizo.

 

Akizungumza na wanahabari Kaimu Kamishna Jenerali wa mamlaka hiyo, Wilbert Kaji,  amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Stanley Salvatory Ngowi au Sultan Salvatory Ngowi (24) mkazi wa Tabata Segerea Dar na Jimmy Walter Mlaki (24) mkazi wa Kinondoni, Dar.

Watuhumiwa wakiwa wamepigwa pingu.

Kaji amesema watuhumiwa hao walikamatwa maeneo ya Ubungo-Kibo, Dar, Januari 27 mwaka huu wakiwa na gari aina ya Sienta rangi ya Silva yenye namba za usajili, T 776 DSE.

 

Ameongeza kuwa maofisa wa mamlaka hiyo walifanya upekuzi kwenye gari hilo na kukamata unga ambao baada ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ulithibitika kuwa ni dawa za kulevya aina ya Heroin wenye uzito wa gramu 508.163.

Kamishna Kaji akisisitiza jambo katika tukio hilo .

Pia, katika upekuzi huo, maofisa hao walikamata mzani wa kidigitali  ‘digital scale’ pamoja na nyaraka mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kamishna Kaji watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa.

Ukamataji huo umefanyika kutokana na mtego uliowekwa na mamlaka hiyo maeneo ya Kibo-Ubungo kufuatia taarifa ya uwepo wa wafanyabiashara hao ambapo licha ya kukamatwa watuhumiwa hao,  wenzao wawili walifanikiwa kutoroka.

Wanahabari kazini kuhusiana na tukio hilo.

Kaji aliwaasa wananchi, hususani vijana,  ambao ndiyo kundi kubwa linalodanganyika na kujihusha na dawa za kulevya, kutojihusisha na biashara hiyo kwa namna yoyote ile.

 

Aliongeza kuwa  sheria ya kupambana na dawa hizo hapa nchini sura ya 95, inatoa adhabu kali mpaka kifungo cha maisha kwa atakayebainika kujihusisha na biashara hiyo haramu.

HABARI: NEEMA ADRIAN

PICHA: RICHARD BUKOS/GPL

MARCEL KAHEZA ” SIMBA SIO Wanabebwa Waamuzi Ndio Tatizo”

Leave A Reply