The House of Favourite Newspapers

VIKATUNI VYAMPUKUTISHA MADEE MILIONI 6

0
Hamad Ally ‘Madee’

MSANII wa Bongo Fleva, Hamad Ally ‘Madee’ amefunguka kuwa video yake ya Wimbo wa Sikila ambayo aliifanya kwa mtindo wa katuni ‘animation’ ni miongoni mwa video ambazo zimekula fedha nyingi kutokana na kuchota kiasi
cha shilingi milioni sita hadi kukamilika kwake.

 

Madee ambaye katika wimbo huo amempa shavu msanii kutoka Nigeria, Tekno, amesema gharama hizo zinatokana na aina hiyo ya video kuwa ya juu kuliko video za kawaida ambazo amekuwa wakishuti.


“Ile video ya Sikila ambayo nimetumia animation imenikamua sana kwani hadi kukamilika kwake imetumika shilingi milioni sita, gharama hizo zinatokana na jinsi ya kubuni vile vikatuni hadi vikamilike kwa sababu inachukua muda sana ndiyo maana gharama zake ni kubwa kuliko video ya kawaida.

 

“Aliyekuwa anafanya kazi ya kutengeneza ile animation alitumia kama mwezi hivi kukamilisha jambo ambalo linafanya utumie gharama kubwa kuhakikisha kwa siku zote hizo kila kitu kinakwenda sawa ili kutoa kitu kizuri,” alisema Madee.

STORI: OMARY MDOSE, GPL

Leave A Reply