The House of Favourite Newspapers

Vilio Safari ya Mwisho ya Baba Kanumba; “Msalimie Mwanao” – Video

0

VILIO, simanzi na majonzi vilitawala wakati wa mazishi ya baba mzazi wa aliyekuwa muigizaji maarufu wa Bongo Movies, Steven Kanumba, mzee Charles Kanumba (71) ambaye alizikwa jana, Machi 11, 2020, katika makaburi ya familia yaliyopo katika Kijiji cha Nyakaboja, Nassa, Busega mkoani Simiyu.

Mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali ya mikoa ya Shinyanga na Simiyu walijitokeza kumsindikiza mzee Kanumba katika makazi yake ya milele.

 

Licha ya marehemu Steven Kanumba kuacha marafiki wengi wakiwemo wasanii wenzake wa tasnia mbalimbali, lakini hakuna staa yeyote wa Bongo Movies au Bongo Fleva aliyeonekana msibani kwa baba Kanumba, jambo ambalo baadhi ya waombolezaji walidai kuwa wasanii hao ni kama wamesusia msiba huo.

 

Mwili wa mzee Kanumba uliagwa juzi Jumanne, Machi 10, 2020, nyumbani kwake  Mtaa wa Magadula, Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, kabla ya kusafirishwa kwenda Simiyu kwa ajili ya maziko.

Charles Kanumba alizaliwa mwaka 1949 huko Busega mkoani Simiyu na alianza kuugua mara baada ya kustaafu kazi serikalini mwaka 2015.

 

Mzee huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya nyonga, tumbo, magoti,  na kibofu cha mkojo, hadi umauti ulipomkuta Machi 8, mwaka huu.

Marehemu Kanumba ameacha mjane  na watoto saba, ambapo alifanikiwa kuzaa watoto tisa, lakini wawili wameshatangulia mbele za haki, watoto wa kiume watano na wa kike wanne.

MWILI WA BABA KANUMBA ULIVYOZIKWA KIJIJINI KWAO NASA BUSEGA!

Leave A Reply