The House of Favourite Newspapers

Viongozi wa Afrika Waungana Kumuaga Kaunda

0

VIONGOZI wa Afrika Julai 2, wamejumuika  na wananchi wa Zambia katika ibada ya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa rais wa kwanza wa taifa hilo, Kenneth Kaunda.

Marais kutoka Ghana, Kenya, na Zimbabwe ni miongoni mwa viongozi wakubwa kutoka Afrika waliohudhuria ibada hiyo ya kumuaga muasisi huyo na mmoja na wapigania uhuru mashuhuri Afrika.

 

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ni miongoni mwa waliohudhuria ambapo mtandao wa Ikulu yake ulichapisha picha za matukio yanayoendelea Lusaka.

 

Kaunda alipigiwa mizinga 21 ya heshima, huku ndege za kijeshi zikiruka juu ya uwanja huko Lusaka kama sehemu ya heshima kwa mkuu huyo wa zamani wa nchi, aliyefariki dunia akiwa na miaka 97.

 

Jeshi la Zambia lilikiupitisha mwili wake katika mikoa 10 ya nchi hiyo ili kuwapa nafasi wananchi kutoa heshima za mwisho.

 

Katika hotuba yake hapo jana kwa taifa hilo, Rais wa Zambia Edgar Lungu,alitoa mapunziko ya siku moja ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi ushiriki kwenye tukio hilo, kupitia televisheni.

 

Kaunda atazikwa Julai 7 mwaka huu katika maziko ya faragha yatakayohudhuriwa na watu wachache wa familia na viongozi wa juu.

Kwa upande wa Tanzania iliwakilishwa na rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan

 

Leave A Reply