The House of Favourite Newspapers

VIONGOZI WA CHUO CHA KIJESHI UGANDA WATEMBELEA EPZA

Viongozi kutoka Chuo cha Uongozi wa Kijeshi cha Kimaka (KDC) cha nchini Uganda wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji (EPZA) kilichoko jijini Dar es Salaam, Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia (hayupo pichani), walipokitembelea leo.
Simbakalia (katikati mbele, suti nyeusi) akiambatana na Mkuu wa Jeshi la Uganda, Andrew Gutti (kushoto) wakati akiwatembeza katika viwanda vilivyoko katika kituo hicho.
Wakiendelea kutembezwa sehemu mbalimbali za kituo hicho.
Simbakalia akifafanua jambo kwa wageni wake baada ya kutembelea sehemu mbalimbali.

VIONGOZI wa chuo  cha Jeshi la Usalama wa Taifa la Kimaka kutoka nchini Uganda (KDC) wametembelea kituo cha Mamlaka ya Uwekezaji (EPZA) kilichoko jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu katika nyanja za uchumi wa viwanda.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho, Kanali Mstaafu, Joseph Simbakalia, amesema kuwa viongozi hao wamejifunza namna ya nidhamu ya kuwapokea wawekezaji inayofanywa nchini na namna ya kuwawezesha kupata leseni za biashara kwa masharti maalum.

Aidha wakati akiongea na waandishi wa habari akizungumzia ujio wa ugeni huo wa Uganda, Simbakalia amewataka Watanzania kuthamini bidhaa zao kwa lengo la kukuza uchumi wa ndani na kuongeza pato la taifa nchini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Uganda, Andrew Gutti,  amesema kuwa wamejifunza kanuni  na mazingira rafiki ambayo yanasababisha ukuaji wa uchumi wa nchi  ukiwemo usalama kwa wawekezaji.

Chuo cha Kimaka kinajumuisha wanafunzi wa mataifa mbalimbali yakiwemo Tanzania, Burundi, Rwanda na Sudan ya  Kusini.

Comments are closed.