The House of Favourite Newspapers

Viongozi Wa DCB Wamtembelea Mama Mkapa na Kumpa Mkono wa Pole

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (wa pili kushoto), Mjumbe wa Bodi, Zawadia Nanyaro na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Rahma Ngassa (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa.
Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa (kulia), akipokea rambirambi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa walipofika nyumbani kwake kumpa mkono wa pole kutokana na msiba alioupata. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Mkapa, Masaki,Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya Benki hiyo, Zawadia Nanyaro pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa.
Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa (kulia), akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro akiushukuru ujumbe wa benki hiyo uliofika nyumbani kwake kumpa mkono wa pole.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa (kushoto) akizungumza na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa (kulia), walipofika nyumbani kwake kumpa mkono wa pole kutokana na msiba alioupata.
Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, marehemu Benjamin Mkapa, Mama Anna Mkapa (kulia), akipokea nishani yenye ujumbe wa maneno ya Rais Mkapa kuhusu uanzishwaji wa benki ya Biashara ya DCB kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Benki hiyo, Zawadia Nanyaro wakati yeye, Mkurugenzi Mtendaji, Godfrey Ndalahwa (katikati) pamoja na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano, Rahma Ngassa, walipofika
nyumbani kwake kumpa mkono wa pole kutokana na msiba alioupata. Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Mkapa, Masaki, Dar es Salaam leo.

 

Leave A Reply