Viongozi Wa UWT Taifa Msibani Kwa Lowassa, Karimjee Dar Es Salaam – Picha
Viongozi wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wakiongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda wamewasili katika Viwanja vya Karimjee,Posta Jijini Dar es Salaam tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Ngoyai Lowassa.
Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndg. Zainab Khamis Shomari, Katibu Mkuu Ndg. Jokate Urban Mwegelo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Taifa Ndg. Hawa Ghasia.