The House of Favourite Newspapers

Viongozi Wafika Kwenye Msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba

VIONGOZI mbalimbali kutoka katika taasisi  binafsi na Serikali, mapema leo  wameendelea kujitokeza kuwafariji ndugu, jamaa na wafanyakazi wa Clouds Media Group,  kwenye msiba wa Marehemu Ruge Mutahaba, nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo (kulia), akizungumzia jinsi uhusiano wake na marehemu Ruge Mutahaba ulivyokuwa kabla ya kufikwa na umauti, mahijiano hayo yamejiri mapema leo baada ya kuhojiwa na kituo cha Clouds TV, nyumbani kwao na marehemu Mikochezi jijini Dar es Salaa.
Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group baada ya kukutana katika msiba wa Ruge Mutahaba nyumbani kwao Mikochezi jijini Dar es Salaam, mapema leo.
Msanii wa vichekesho, Joti (kulia), akisalimiana na Mh. Nape Nnauye.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga (kulia), akisalimiana na Mh. Nape Nnauye.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga.
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Jakaya Kikwete (katikati), akisaini kitabu cha maombolezo, huku akishuhudiwa na mkewe Mama Salima Kikwete (kushoto) na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza, mara baada ya kuwasili kwenye msiba wa Ruge Mutahaba nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar, mapema leo.
Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe (katikati), akiteta jambo na Mbunge wa Sengerema mjini William Ngereja (kulia) huku Mbunge wa Iringa Iringa mjini Peter Msigwa, baada ya kukutana katika msiba wa Ruge Mutahaba nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar, mapema leo.
Mkurugenzi wa Global Group, Eric Shigongo (kushoto), akiteta jambo na Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe, baada ya kukutana kwenye msiba wa marehemu Ruge Mutahaba, nyumbani kwao Mikocheni jijini Dar es Salaam, mapema leo.
          

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA/GPL

 

Comments are closed.