The House of Favourite Newspapers

Viporo vya Simba vyazua maswali Yanga

KITENDO cha Yanga juzi Jumapili kucheza mechi yake ya 15 katika Ligi Kuu Bara huku Simba ikiwa na mechi 12, kimezua maswali mengi huku lawama za Yanga zikienda kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (TPLB).

 

Simba ikiwa imecheza mechi 12, inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikijikusanyia pointi 27, huku Yanga ikiwa na pointi 38 kabla ya mechi ya jana dhidi ya Biashara United.

Hivi sasa Simba ina michezo mitatu nyuma ya Yanga kutokana na kushiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Desemba 15, mwaka huu itacheza ugenini dhidi ya Nkana ya Zambia kabla ya kurudiana Desemba 21 jijini Dar.

 

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, amehoji kisa cha wapinzani wao kutocheza mechi yoyote ile kwa wiki mbili nzima baada ya wao kurudi kufuatia kucheza mechi yao ya kimataifa dhidi ya Mbabane Swallows.

“Yanga wakati tupo tunacheza michezo ya Kombe la Shirikisho tuliporudi kutoka Kenya siku mbili tunaenda Shinyanga siku mbili baada ya hapo unaenda Mbeya baada ya siku tatu tunaenda Rwanda.

 

“Simba wamecheza hapa juzi ligi lakini hawajacheza mechi yoyote ile kwa wiki mbili wakiajiandaa na mechi ya kimataifa kwa sababu gani? Hilo ni jambo la ovyo, hatuendi kuendesha mpira kwa namna hiyo,” alisema Zahera.

Ikumbukwe kuwa, malalamiko hayo ya Yanga juu ya viporo vya Simba, hata Simba nao waliwahi kuwalalamikia TFF na Bodi ya Ligi kipindi Yanga inashiriki michuano ya kimataifa.

SAID ALLY, Dar es Salaam

Comments are closed.