The House of Favourite Newspapers

Virusi Vipya vya Corona Vyaua Watu China

0

KAMATI ya Dharura ya Shirika la Afya Duniani (WHO), itakutana wiki hii kujadili mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vipya vya aina ya Corona.

 

Homa hiyo inayofananishwa na ugonjwa wa SARS unaosababisha ugumu wa kupumua, imeenea zaidi China.

Mtaalamu mmoja wa afya kutoka China amesema ugonjwa huo unaweza kuambukiza kutoka mwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine.

 

Na hadi sasa maofisa wa afya wamesema mtu mmoja amefariki leo katika mji wa Wuhan, eneo la kati nchini China, kutokana na mlipuko wa ugonjwa huo na hivyo kuongeza idadi ya waliokufa kufikia watu wanne huku idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo vipya imeongezeka hadi watu 218.

Mlipuko huo ulioanzia mji wa Wuhan umesambaa katika miji kadhaa ya China ukiwemo mji mkuu Beijing na Shanghai.

Leave A Reply