The House of Favourite Newspapers

Virusi Vipya vya Corona Vyazua Hofu Uingereza

0
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson

WAZIRI Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema utafiti wa awali unaonyesha kuwa virusi vipya vya ugonjwa wa corona vilivyojitokeza Uingereza ndio hatari zaidi.

 

Data hiyo imetokana na kulinganishwa kwa idadi ya vifo kati ya watu waliopata maambukizi na virusi vipya ama vile vya zamani vya corona,maambukizi yanayosababishwa na virusi vipya tayari yamesambaa kote Uingereza.

 

Johnson amesema katika taarifa: kuwa mbali na kwamba vinasambaa kwa haraka, sasa hivi pia inaonekana  kwamba kuna ushahidi kuwa virusi vipya vile ambavyo mara ya kwanza kabisa vimebainika London na kusini mashariki – huenda vikasababishwa vifo vya watu wengi.

 

“Athari kubwa imetokana na virusi hivyo vipya na hilo linamaanisha wizara ya afya sasa hivi inakumbana na shinikizo kubwa.”

 

Kundi lililokuwa linafanya utafiti, limehitimisha kuwa “kuna uwezekano mkubwa” virusi hivyo vimekuwa hatari mno.

 

“Nataka kusisitiza kuwa bado kuna sintofahamu kuhusiana na idadi na juhudi zaidi zinahitajika lakini bila shaka inatia wasiwasi kwamba virusi hivyo vimechangia ongezeko la idadi ya vifo pamoja na kiwango chake cha maambukizi.”amesema Boris.

 

Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa virusi vipya vinasambaa kwa asilimia 30 na 70 haraka zaidi ya virusi vyingine na inasemekana kuwa ni hatari zaidi kwa asilimia 30.

 

Virusi hivyo vipya mara ya kwanza vimebainika Kent mnamo mwezi Septemba na sasa hivi vinapatikana kwa nchi nyingi na  maeneo ya England na Ireland Kaskazini.

Leave A Reply