The House of Favourite Newspapers

Vita ya Ngumi za Kimataifa Mubashara Global TV

0

Vita ya Ngumi za Kimataifa vitaoneshwa Mubashara na Global TV JULAI 22, mwaka huu katika Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. Vumbi la aina yake litatimka siku hiyo wakati mabondia watatu wa kimataifa watakapokuwa wakizichapa kugombania Mkanda wa Ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati.

Mapambano hayo ambayo yatarushwa mubashara na Televisheni ya Mtandaoni ya Global TV Online BURE, yatakuwa kama ifuatavyo:

Chichi Mawe

CHICHI MAWE VS ISRAEL KAMWAMBA

Chichi Mawe ambaye amecheza jumla ya mapambano 62, akishinda 41, 24 yakiwa ni KO, amepoteza 17 kati ya hayo 14 ni kwa KO na ametoka sare manne huku pambano lake la kwanza akicheza mwaka 1998. Kamwamba ni mpinzani wa Chichi Mawe ambaye ana rekodi ya kucheza mapambano nane na yote ameshinda, matano yakiwa kwa KO.

Rekodi zinaonyesha ni bondia ambaye ni moto wa kuotea mbali kufuatia kukaa juu ya ringi kwa raundi 34. Utamu wa pambano hili unatokana na tofauti ya staili ya miguu wanayotumia mabondia hao, Chichi Mawe ni Southpaw yaani  anatanguliza mguu wa kulia mbele wakati Kamwamba ‘Israel Mweusi’ ni Orthodox yaani anatanguliza mguu wa kushoto mbele, hivyo hapo ushindani wa kimataifa utaonekana kwa kuwa kila mmoja anahitaji kuchukua ubingwa.

Nasibu Ramadhan ‘Pacman’

NASIBU RAMADHAN VS TINASHE MWADZIWANA

Nasibu Ramadhan ‘Pacman’ huenda akawa hajulikani sana na mashabiki wengi kama ilivyo kwa Francis Cheka na Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, lakini kwa wale

ambao wamekuwa mara nyingi wakimuona ndani ya ringi ni moto wa kuotea mbali kutokana na staili yake anayotumia  iliyosababisha apewe jina la mkali wa kutoka nchini Ufilipino,  Manny Pacquao ‘Pacman’.

Nasib Ramadhani Nitampiga vibaya Mzimbabwe Njooni Dar Live

Pacman wa Bongo ambaye atacheza na Mzimbabwe, Tinashe Mwadziwana katika pambano la ubingwa wa Global TV, Afrika Mashariki na Kati, rekodi yake ni moto wa kuotea mbali licha ya kuwa na umbo dogo ambalo unaweza kuamini hawezi kutoa ushindani.

 

Tinashe Mwadziwana – ZIMBABWE

Bondia huyo amecheza mapambano 33, ameshinda 22, kati ya hayo, 11 ameshinda kwa KO. Kwa aliyopoteza, jumla ni tisa ambapo matatu ni kwa KO, huku akitoka sare mawili. Rekodi hiyo ambayo sawa na raundi 33 zenye dakika 99, zinaonyesha ni wazi Pacman siyo bondia wa mchezo licha  ya mpinzani wake kuwa na rekodi ya kushinda mapambano 12, sita ni kwa KO, akipigwa 12 moja ni  kwa KO, hivyo imemfanya acheze jumla ya mechi 24, sawa na raundi 129. Mwadziwana anayetambulika kwa jina la utani la The Chairman, atakuja nchini kwa lengo moja tu la kupambana na Pacman ambaye siku zote huwa ngumu kwake kupigika kirahisi tena akiwa anaiwakilisha nchi kwenye vita hiyo itakayo-muhusisha mtoto wa Rais wa Tanzania,  Dk. John Pombe Magufuli na wa Zimbabwe, Robert Mugabe.  

Huenda pambano hili likazidi kuwa kali kwa kuwa Pacman anatumia mtindo wa ‘Southpaw’ kutanguliza mguu wa kulia mbele, wakati wa kushambulia, huku mpinzani wake staili yake imebaki kufanywa siri kitendo kitakachomfanya atumie akili nyingi kuhakikisha anaibuka na ushindi.

 

IDD PIALALI (TANZANIA)  VS REGIN CHAMPION (MALAWI)

Pialali anasifika kuwa ni bondia ambaye hachoki akiwa ndani ya ulingo, mashabiki wake wanadai kuwa ana mapafu ya mbwa kutokana na uwezo wake wa kutupa vitasa vikali huku akiwa anatembea, anatajwa kuwa ndiye mrithi sahihi wa marehemu, Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’.

Pialali anarekodi ya kushinda mapambano 20, 15 yakiwa ni KO, amepigwa katika mapambano matatu huku akitoka sare moja, bondia huyo mwenye mbwembwe ndani ya ulingoni, anatumia mguu wa kulia ‘Orthodox’. Wakati mpinzani wake kutoka nchini DR Congo, Regin Champion ameshinda mapambano 15, kati ya hayo 13 ni kwa KO na mawili kwa pointi, huku akipoteza manne.

Idd Pialali: Njooni Dar Live Mshuhudie Nitakavyomuua Mkongo

 Katika hatua nyingine, pambano hilo  la Ngumi za Kimataifa halitakuwa na kiingilio na mashabiki wataweza kulishuhudia mubashara (LIVE)  kupitia simu zao za mkononi tu, kwani litaoneshwa na  Global TV pekee. Wadau na mashabiki watakaopata nafasi ya kuingia ukumbini wataingia kwa kadi maalum za mwaliko tu.

Ili kulishuhudia pambano hilo kwa njia ya simu tena BURE, HAKIKISHA unajiunga (SUBSCRIBE) na YouTube Chanel ya Global TV Online sasa hivi ili usipitwe. Ingia You Tube, tafuta GLOBAL TV ONLINE, kisha bonyeza neno SUBSCRIBE pia bonyeza kikengele kidogo kilichopo pembeni yake ambacho kitakukumbusha kuangalia pambano hilo mara tu litakapoanza.

Kama wewe umeshajiunga, basi hakiksha pia umebonyeza kikengele ili usipitwe na kila kinachoendelea Global TV. Pia unaweza kutupata kupitia mtandao wetu wa www. globaltvtz.com.  Usisubiri, jiunge sasa na Global TV ili uwe wa kwanza kuona ndondi za kimataifa. KAJIUNGE SASA kwa kubonyeza HAPA: https://www.youtube.com/user/uwazi1

Leave A Reply