The House of Favourite Newspapers

Vita Ya Malkia wa Bongo Fleva Zuchu na Esma Yafika Pabaya Diamond Atajwa Kuwa Chanzo

0
                                     Dada wa msanii , Diamond Platnumz Esma Platnumz.

ZUHURA Othman Soud almaarufu Zuchu au Zuuh; ni malkia mpya wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye anadaiwa kuingia kwenye vita nzito na dada wa bosi wake, Diamond Platnumz aitwaye Esma Platnumz.

 

Waja wanasema kuwa, vita ya Zuchu na Esma imefika pabaya kwani wamefikia hatua ya kuondoana kabisa urafiki kwenye mitandao ya kijamii.

 

Hatua hiyo inakuja wakati huu ambapo Zuchu anadaiwa kuzama mazimamazima kwenye penzi na Diamond au Mondi wakati Esma na baadhi ya memba wa familia hiyo akiwemo Mama Dangote hawataki kusikia jambo kama hilo, badala yake wanamtaka mtangazaji Aaliyah.

Zuchu; hata hivyo, baada ya kuona mambo yanakuwa mengi, amejitokeza na kuweka wazi kuwa uhusiano kati yake na dada huyo wa bosi wake bado ni mzuri.

 

“Sina bifu na Esma, sina ugomvi naye. Kila siku anasapoti nyimbo zangu na hata kwenye group la ofisi anaandika kwamba mimi ni msanii anayemkubali.

 

“Pia yeye ni dada wa bosi wangu kwa hiyo siwezi kuwa na bifu naye kabisa,” anasema Zuchu.

Leave A Reply