Vodacom Tanzania yaja na kampeni ya ‘life is better’

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(watatu toka kushoto)akiwa ameshikana mikono na baadhi ya viongozi wa taasisi zilizowezeshwa na Kampuni hiyo kufanya wanajamii maisha yao kuwa murua.Wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni hiyo ya“Life is better” inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi kwa kutuma na kupokea pesa kwa M PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto katika picha Msimamizi wa kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts,Mmoja wa akina mama aliyepona Fistula Cherry Msangi,Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi na Mkuu wa Vodacom Foundation,Renatus Rwehikiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao(kushoto)akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa walemavu wa hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni mpya ya kampeni hiyo “Life is better” inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi ,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa akina mama aliyetibiwa na kupona Fistula katika hospitali ya CCBRT, Cherry Msangi akitoa ushuhuda kwa waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi wa kampeni mpya ya Vodacom Tanzania ya” Life is better” inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam,Wengine katika picha ni Msimamizi wa kituo cha Mabinti Centre,Katia Geurts na Mkurugenzi wa walemavu katika Hospitali ya CCBRT,Brenda Msangi(kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao akiongea na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya “Life is better inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao(hayupo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni mpya ya kampuni hiyo ya “Life is better inayolenga kuendelea kunufaisha jamii kwa kutoa intanet yenye kasi zaidi na kutuma na kupokea pesa kwa M-PESA kwa haraka na salama zaidi ,Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania,Ian Ferrao amezindua kampeni mpya ya  kampuni hiyo inayojulikana Kama ‘Life is Better,’katika hafla iliyofanyika jijini Dar esk Salaam.Kampeni hii inadhihirisha ni kwa jinsi gani Vodacom imeweza kuleta mabadiliko kwenye jamii ya watanzania tangu ianze kutoa huduma nchini, pamoja na mafanikio hayo  mwaka 2016 imejizatiti kuendelea kuleta mabadiliko makubwa kwa kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia,”alisema Ferrao na kuongeza kuwa kampuni inajivunia kutoa huduma za maongezi na intanet yenye kasi kubwa ambazo zinawezesha wateja kuzitumia kubadilisha maisha yao na kubuni fursa mpya.
Ikiwa ni kampuni inayoongoza kwa kuwa na mtandao mkubwa nchini mwaka wa 2015 imepata mafanikio makubwa kwa kuanzisha huduma mbalimbali  ambazo zimegusa maisha ya watanzania wengi katika kuzitumia na zinazidi kuwarahishia maisha na zimewawezesha kuingia katika ulimwengu wa  teknolojia.
“Mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa ambapo Vodacom imeweza kubuni huduma  za kuboresha maisha ya wateja wetu kupitia mawasiliano na hii imetokana na mkakati wa kampuni wa kuwekeza katika miundombinu  ya mawasiliano,wafanyakazi wake na kwenye ubunifu wa kiteknolojia na ndio maana  imeweza kuanzisha huduma mbalimbali  za kuwarahisishia maisha wateja wake ambazo wanaendelea kuzifurahia”.Alisema
Hadi sasa, Vodacom imewekeza dola za Marekani bilioni moja, na imejenga mtandao wa kutoa huduma za intaneti za 2G na 3G unaowafikia asilimia 87 ya Watanzania nchini kote na imeongeza idadi ya wateja wake  kufikia ziadi ya milioni 12.
Alisema mwaka wa 2015 ulianza kwa Vodacom kuanzisha promosheni kubwa ya JayMillions  iliyokuwa inatoa  nafasi ya washiriki kujishindia hadi shilingi milioni 100 kwa siku na wateja walioshiriki na kushinda maisha yao yamebadilika na kuwa bora na kufanikiwa kutimiza ndoto  zao .
“Promosheni ya JayMillions imebadilisha maisha ya washindi kwa ndoto zao kutimia,wapo ambao wameendeleza biashara zao,wapo ambao wamejiendeleza kielimu,wao waliojenga nyumba na kuanzisha biashara.Tunajivunia kushiriki katika hatua ya kubadilisha maisha yao kutokana na zawadi za fedha walizojishindia kupitia promosheni hii.”Alisema Ferrao.
Mafanikio mengine ya kampuni aliyabainisha kuwa ni kuzidi kukua kwa Huduma ya M-Pesa inayotumiwa na watanzania  zaidi ya wateja  milioni 7 nchini na ikiwa na mtandao wa mawakala zaidi ya 85,000 nchini kote imevuka mipaka ya nchi kwa ushirikiano na Kampuni za Safaricom ya Kenya na MoneyGram  ambapo hivi sasa mteja anaweza kutuma na kupokea fedha kutoka nje ya nchi kupitia huduma hii,vilevile huduma ya kujiwekea akiba na kukopa kwa urahisi kupitia simu ya mkononi ya M-Pawa imezidi kuimarika,kuaminiwa na kutumiwa na wateja wengi.
“Zaidi ya wateja milioni 1.5 wanatumia  huduma hii wakiwa wameweka akiba inayofikiashilingi bilioni 6.8 na mikopo inayofikia milioni 500 inatolewa kwa wateja,huduma imechangia kuwezesha watanzania wengi kuweza kupata huduma za kibenki”.Alisema.
Huduma zinginezo ambazo zimeanzishwa na kuendelea kufurahiwa na watumiaji wake baadhi yake alizitaja kuwa ni kampeni ya RED,Spend and Get.Huduma ya RED inawarahishia maisha wateja wenye shughuli nyingi ambapo wanapata kifurushi maalumu na kupata huduma zote za mawasiliano kwa gharama nafuu na M-Pesa wakati huo huo  wanajipatia ofa ya kurejeshewa  asilimia 10%kupitia akaunti zao za M-Pesa.
Vilevile alizitaja huduma za kuleta furaha na burudani kwa wateja  kama vile Ishi Kistaa na Mziiki ambazo zinawawezesha wateja kusikiliza muziki kutoka kwa  wasanii mbalimbali kupitia simu zao za mkononi  na kuhusu michezo  kampuni inaendelea kuwa mdhamini wa ligi  ya soka nchini.
Pia aliitaja huduma ya Kilimo Klub ambayo imelenga kuboresha maisha ya wakulima na kuongeza uzalishaji ambapo wakulima wengi hususani wanaoishi vijijini wanaendelea  kuifurahia kwa kuweza kupata mikopo yenye masharti nafuu ya M-Pawa ambayo hasa imewalenga wao ikiwemo kupata taarifa za hali ya hewa na bei za mazao kwenye masoko. “Vodacom itaendelea kufanya ubunifu wa  huduma za aina mbalimbali ambazo zitawarahishia maisha zaidi na kuwafikia watumiaji wengi wa simu za  mkononi tofauti na sasa ambapo wapo baadhi hawazipati”.Alisema
Vilevile alibainisha kazi kubwa iliyofaywa na taasisi ya kuhdumia masuala ya kijamii ya Vodacom Foundation katika  kuleta mabadiliko kwenye jamii ambapo kwa mwaka huu ilijikita zaidi kutoa misaada mbalimbali kwa jamii  nchini kote hususani  kwa upande wa elimu , afya  na makundi mbalimbali yenye mahitaji.
Mwaka huu imewezesha operesheni kwa ajili ya wanawake 1,000 walioathirika na fistula, kuwezesha wasichana  kubaki shuleni kupitia mradi wa Hakuna Wasichoweza  ,kusaidia wahanga wa ugonjwa Sickle Cell,Saratani,huduma ya uzazi kwa akina mama ya ‘Wazazi Nipendeni,kuendesha kampeni za Usalama barabarani na kuwezesha zaidi ya wanafunzi  kusoma elimu ya kompyuta kwa vitendo mashuleni,kufadhili kituo cha MABINTI kinachotoa mafunzo kwa wanawake waliopona ugonjwa wa Fistula “Dhamira yetu kubwa ni kuona tunatokomeza ugonjwa wa Fistula nchini na kukabuliana na changamoto mbalmbali zilizopo katika sekta ya afya na elimu”.Alisema.
Mwaka huu  umekuwa wa mafanikio na Vodacom imeweza  kubadilisha maisha ya maelfu ya watanzania kuwa bora na imejizatiti na kujipanga  kupitia kampeni hii ya Life is Better kuendelea kufanya vizuri mwakani lengo kubwa likiwa ni kutimiza dhamira yake ya kubadilisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia na kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Katika mwaka ujao itaendelea kubuni huduma mbalimbali za kuboresha maisha ya watanzania kupitia teknolojia ikiwemo kuwawezesha watanzania wengi kuunganishwa na  huduma za internet na kuwadhihirishia jinsi huduma hii ni ya msingi kwa kubadilisha maisha ya watu na kujenga Tanzania  iliyo bora katika miaka ijayo.

Loading...

Toa comment