The House of Favourite Newspapers

Vodacom Tanzania Yatoa Msaada wa Vifaa vya Tehama Jijini Dodoma

0

VODACOM Tanzania Plc kupitia Vodacom Tanzania Foundation, inaendeleza juhudi za kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali, ambapo jana imekabidhi msaada wa vifaa vya Tehama kwa shule ya Sekondari Dodoma. Angalia picha za matukio;

MKURUGENZI Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire na mkuu wa shule ya sekondari Dodoma Francis Tumaini wakifungua pazia ili kuzindua darasa la Tehama ambalo limewekewa vifaa na kampuni hiyo, vifaa hivyo ni Kompyuta 15, Meza 15, viti 15, Televisheni moja, kifushi cha intaneti kwa mwaka mmoja ambapo msaada huu umegawiwa ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kidijitali lakini pia kuwawezesha wanafunzi kusoma somo la Kompyuta ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada za serikali za kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire akimuuliza swali dada mkuu wa shule ya sekondari Dodoma kuhusu namna ‘Coding’ inavyomsaidia katika kujifunza darasani, binti huyo ni mojawapo ya wasichana wanaosoma tahasusi (Combination) mpya ya Fizikia, Hisabati na Sayansi ya Kompyuta (PMC) ambapo msaada uliotolewa na kampuni hiyo utawasaidia katika kujifunza zaidi. Wanaoshuhudia ni wanafunzi wa kike wanaosoma tahasusi hiyo.

 

 

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vodacom Tanzania Plc Philip Besiimire akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo na waalimu wa shule ya sekondari Dodoma mara baada ya hafla ya kukabidhi vifaa vya Tehama shuleni hapo.
Leave A Reply