The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yakabidhi Bima za Afya 200 Kwa Wanawake na Watoto Jijini Mwanza

0
Maryglory Mtika wa Vodacom Tanzania (kushoto) akiwa na mmojawapo wa akina mama na mtoto wake waliopatiwa bima ya bure kwa mwaka mzima katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou-Toure jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu.

 Mshindi wa pesa taslimu shilingi milioni 10 kupitia kampeni ya Vodacom Tanzania PLC inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, Bw. Simon Bundala (wa pili kulia) akiwa ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa na Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) pamoja na msanii wa Bongo Flava, Dogo Janja (wa kwanza kushoto) na Straton Mchau, Meneja Mauzo Mwandamizi Kanda ya Ziwa (wa pili kushoto) katika viwanja vya Posta jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.

 

Masta Shangwe (mwenye kofia ngumu) kutoka Vodacom Tanzania akifurahi pamoja na mmojawapo wa akina mama waliopatiwa bima ya bure kwa mwaka mzima katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Sekou-Toure jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kupitia kampeni yake inayoendelea ya ‘Sambaza Shangwe, Gusa Maisha’, kampuni hii imekabidhi kadi za bima kwa akina mama 100 na watoto 100 hospitalini hapo ikiwa ni zawadi ya upendo kutoka kwa kampuni hiyo katika msimu huu wa sikukuu.

 

Kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom, imetoa bima za afya 200 kwa wanawake na watoto 200 pamoja na zawadi mbalimbali kupitia Kampeni ya Sambaza Shangwe, Gusa Maisha jijini Mwanza.

Kupitia kampeni hii wateja wanayo fursa ya kushinda zawadi mbalimbali ikiwemo bodaboda, luninga, simu za mkononi, router za 4G na 5G pamoja na pesa taslimu kila wiki kuanzia shilingi laki tano mpaka milioni 10 kwa kununua vifurushi, kufanya malipo kwa M-Pesa na kupakua DJ Mixes kupitia Mdundo.

Leave A Reply