The House of Favourite Newspapers

Hanang, Tigo Watoa Msaada Wa Mahitaji Muhimu Kwa Waathirika

0

Meneja Wa Tigo, Kanda ya Kaskazini akikabidhi msaada kwa mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja, Hanang jana.

Manyara 18 Desemba 2023: Wafanyakazi wa Tigo kwa pamoja wametoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na vifaa kwa Waathirika wa Mafuriko yaliotokea tarehe 02 Desemba 2023 katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara. Akikabidhi Vifaa hivyo Meneja wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Daniel Mainoya alieleza namna walivyoguswa na tukio hili na ndio maana walifikia maamuzi ya kutoa msaada kusaidia Waathirika hao.

Akitoa shukrani, Mhe, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Bi. Janneth Mayanja alisema kuwa msaada uliotolewa na Tigo umegusa Waathirika kwa kiasi kikubwa sana hasa kwa kuzingatia mahitaji ya waathirika,haswa magodoro yatakayo weza kutatua swala la malazi. Aliendelea kwa kuhamasisha Taasisi nyingine na Watu binafsi kuiga mfano wa Tigo, kuja kujitolea kwa chochote watakachojaaliwa                    

Magodoro nayo yalikuwa sehemu ya msaada huo.   

Leave A Reply