The House of Favourite Newspapers

Vodacom Yarudisha Kwa Jamii Ikiwa Ni Sehemu Ya Kusaidia Yatima Na Watoto Wenye Mazingira Magumu

0
Mkurugenzi wa kituo Cha kulelea watoto yatima cha KIWALANI ORPHAN CENTER akipokea vitabu kutoka kwa Mkurugenzi wa Tehama Vodacom Athumani Mlinga akiwa na Mkurugenzi Rasilimali watu Vodacom Vivienne Penessis.

Kampuni ya Vodacom Tanzania imetoa vitu mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima na waishio kwenye mazingira magumu kiitwacho KIWALANI ORPHAN CENTER kilichopo Kiwalani jijini Dar es Salaam ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi Tehama kutoka Vodacom, Mr.Athumani Mlinga amesema kuwa mchakato huo ulifanyika ambapo kila mwaka Vodacom na Vodaphone Ulimwenguni Kuna utaratibu wa kushirikisha wafanyakazi na kuwashindanisha kila mwaka wanatoa changamoto ya afya kwa wafanyakazi hivyo basi wanakuwa na utaratibu wa kufanyika matukio mbalimbali kujenga afya kwa wafanyakazi.

Mkurugenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima Cha KIWALANI ORPHAN CENTER akiwa amekalia Moja ya kiti ambavyo vimetolewa na Kampuni ya Vodacom Tanzania.

“Katika ushindanishwaji huo Vodacom Tanzania imekuwa ni mshindi wa tatu ikiwa ni kila mfanyakazi anashiriki katika mashindano iwe ni kutembea au kukimbia na kutoka jasho.

“Katika kushinda huko kunapatikana zawadi ya fedha hivyo basi tukaona tutoe kwa watu wenye uhitaji,tukaona tuleta vitu ambayo vitawasaidia watoto hawa katika masomo Yao,” amesema Mlinga.

Watoto hao wakiwa pamoja na wafanyazi wa Kampuni ya Vodacom Tanzania wakiwa kituoni hapo.

Vitu ambayo Kampuni hiyo imetoa katika kituo hicho ni pamoja na vitanda 15 vya double,magodoro 30, viti na meza za kukalia watoto 40,vitabu 322, Computer ya mezani 1, viti vya ofisi 5 pamoja na vitu mbalimbali vyenye dhamani ya shilingi milioni ishirini na Moja laki mbili na elfu sitini na tano ( 21,265,000,00.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa na Kampuni ya Vodacom Tanzania ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii.

Nae Mkurugenzi wa KIWALANI ORPHAN CENTER,Much.Elias Mwakalukwa amesema kuwa amewashukuru Kampuni ya Vodacom kwa kuja kituoni hapo kwa kuwa ni bahati kubwa sana kwa upande wao.

Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kituo hicho.

“Mimi nashukuru sana kwa kutudhamini Kuna vituo vingi lakini mmechagua kituo chetu naamini Mungu ametenda haya hivyo basi tunaushuru uongozi mzima wa Vodacom kwa msaada huu mkubwa uliyotuletea kwa watoto wetu hawa ambayo hawana wazazi na wengine wanaoishi kwenye mazingira magumu,hivyo nawaahidi kuvitunza vile vyote ambayo mmetuletea na watoto watasoma vizuri na watapata ufaulu mzuri,”amesema Mch.Mwakalukwa.

Leave A Reply