Vodacom Yatoa Mafunzo ya TEHAMA kwa Vikundi Mbalimbali Jijini Dar es Salaam
Afisa Utumishi kwa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akitoa zawadi kwa mwakilishi wa kikundi cha Tanzania Safari Adventures Keziah Mafuru baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na kampuni hiyo kupitia taasisi ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.