The House of Favourite Newspapers

Bad News: Wafanyakazi wa Ayo TV Wapata Ajali, Wawili Wafariki

0
Nelly enzi za uhai wake.

TAARIFA iliyotufikia hivi punde ni kwamba wafanyakazi wawili wa Ayo TV mkoani Mwanza, wanaofahamika kwa majina ya Dullah TZA na Nelson Brigeri ‘Nelly TZA’ pamoja na mwenzao mmoja (ambaye si mfanyakazi wa Ayo TV) aliyefahamika kwa jina la Mujitaba Abbas wamepata ajali maeneo ya Kibaha usiku wa kuamkia leo Jumatano, Agosti 18, 2021 wakati wakiwa safarini kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam.


Taarifa zinaeleza kuwa ndani ya gari hilo dogo binafsi kulikua na watu watatu ambapo wawili wamefariki dunia (Nelly ambaye ni mfanyakazi wa Ayo TV) na Mujitaba (ambaye hakuwa mfanyakazi wa Ayo TV).

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Ayo TV, Dar es Salaam, miili ya marehemu imeifadhiwa Hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani ambapo pia Dullah aliyepata majeraha anaendelea na matibabu.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers na Global TV Online tunatoa pole kwa Mkurugenzi wa Ayo TV, Millard Ayo, wafanyakazi wote wa Ayo TV, ndugu pamoja na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Nelly mahali pema peponi, AMEN!

Leave A Reply