The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaifunga Majimaji bao 1-0

yanga-2

Kikosi cha timu ya Yanga Kilichoanza dhidi ya timu ya Majimaji leo katika Uwanja wa Majimaji, Songea.   

Mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho na mpira umekwisha. Yanga wanaondoka na pointi 3 muhimu kwa kuichapa Majimaji bao 1-0.

Dk 90: Yanga wanafanya mabadiliko tena, Oscar Joshua anaingia kuchukua nafasi ya Kapteni Haruna Niyonzima.

Dk 87: Haruna Niyonzima anaondoka anaachia krosi maridadi inamkuta Juma Mahadhi anakosaaa.

Dk 80: Yanga wanafanya mabadiliko hapa, Deus Kaseke anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Said Juma.

yanga-14

Mashabiki wa timu ya Yanga wakishangilia.

Dk 76: Yanga wanaingia langoni mwa mMajimaji, Kaseke anampa Juma Abdul,

Dk 75: Wanakwenda tena Majimaji, inachezwa krosi kali hapa lakini Dida anawahi na kutoa mkwaju huo.

Dk 73: Majimaji wanapata faulo langoni mwa Yanga lakini wanapiga nje na inakuwa goal kick. Wanakosa umakini wa mchezo hawa Majimaji.

Dk 72: tayari Majimaji wamekwisha anza na wanaliskama lango la Majimaji lakini Goal Keeper Dida anauwahi mpira.

Dk 72: mahadhi anakwenda tena lakini anafanya maamuzi ya haraka anakosa bao. Walinzi wa Majimaji wanaonekana kukosa kuelewana hap.

yanga-3

Kikosi cha timu ya Majimaji kilichoanza dhidi ya Yanga.

Dk 70: Kaseke anaingia na mpira, anakosaaa, Juma Mahadhi alikuwa kwenye position ya kufunga lakini uchoyo wa Kaseke unawakosesha Yanga bao la wazi.

Dk 62: Yanga wanafanya shambulizi kali, Msuva anashindwa kutumia nafasi anayopata akiwa mbele ya lango la Majimaji.

Dk 59: Majimaji wanafanya mabadiliko, anatoka Yakub Abdallah anaingia Paul Nyangwe.

Dk 59: Yanga wanashambulia tena, Tambwe anapokea pasi nzuri ya Msuva na kuinuka nayo langoni lakini anakosa.

Dk 57:  Mpira umesimama baada ya Yondani kufanyiwa madhambi na kuumia. Anatibiwa hapa.

Dk 54: Haji Mwinyi anampasia Msuva, anaondoka na mpira na kumgonganisha mchezaji wa Majimaji inakuwa kona kuelekea kwa Wanalizombe.

yanga-4

Dk 50: Tambwe anachezewa faulo, anapiga Haji Mwinyi, hakuna mtu, golikipa Agaton Anton anawahi mpira huo.

Dk 48: Yanga wanaingia tena langoni mwa Majimaji, Msuva anakosa bao hapa.

Dk 46: Semwanza anapigwa kadi ya njano baada ya kumvuta Msuva. Faulo anapiga Haji Mwinyi

Dk 45: Majimaji wanafanya mbadiliko mengine, Peter Mapunda anaingia kuchukua nafasi ya Lukas Kikoti.

Dk 45:Mpira umeanza kipinda cha pili

yanga-12

Dk 45 +2: MPIRA NIMAPUMZIKO

Inavyoonekana Yanga wanatengeneza mashambulizi yao kupitia viungo wa kati na pembeni ambako kuna Simon Msuva. Tambwe anaoongoza vizuri idara ya ushambuliaji na kuwazidi uajanja Majimaji. kukosekana kwa Alex Kondo kwa klabu ya Majimaji ambaye ana kadi 3 za njano na nafasi yake kuchukuliwa na chipkizi, Kibinga kutoka Academy ya Kigamboni, anayeonekana kuzidiwa na wakongwe akina Tambwe.

Yanga wanaonekana wepesi kufunguka, wanajiamini, wamecheza mechi nyingi kubwa kwa wiki ukilinganisha na Majimaji.

Dk 45: Zinaongezwa dakika 2.

Dk 44: Yanga wanaingia tena hapa, wanakosa bao la wazi kabisa. Inavyoonekana mabeki wa Majimaji Kipepe na Mwakinyuki wamezidiwa mashambulizi ya Yanga.

Dk 40: Yanga wanakwenda tena, Msuva anaingia na mpira, Majimaji wanatoa inakuwa kona. Tayari kona inapigwa lakini Majimaji wanaondosha langoni mwao.

Dk 37: Yanga wanaingia langoni mwa Majimaji, Tambwe anaingiza mpira langoni, refa anasema ni offside.

Dk 35: Piga nikupige kwenye lango la Yanga, Majimaji wanakosa bao la wazitena. Wanamzonga mwamuzi hapa.

Dk 33: majimaji wamezinduka, wanalisakama lango la Yanga, wnapeleka mashambulizi haswa.

Dk 31: George Mpole anaingia langoni mwa Yanga, lakini mpira unatoka na kuwa kona, Majimaji wanacheza kona hiyo na Mpole anakosa bao la wazi mpira unakuwa goal kick langoni mwa Yanga.

Dk 27: Majimaji wanajaribu kupeleka shambulizi langoni mwa Yanga lakini wanashinwa kufanaya maamuzi sahihi ya kuweza kuwasaidia kuwapa bao. Majimaji wanafika langoni kwa Yanga lakini kipa Dida anauwahi mpira. Wanaonekana kupoteza nafasi nadhani ni kwa sababu ya hofu na kupaniki kwa kuanziwa bao.

yanga-5

Dk 24, Majimaji wanafanya mabadiliko, anatoka Bahati Yusufu na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Semwanza.

Dk 17, Mpira umekuwa ni wa kasi sana, Kamusoko anawekwa chini hapa, Majimaji wanaonekana kulinda lango lao hivyo kuwapa mwanya Yanga kulishambulia lango hilo mara kwa mara.

Dk 16, Yanga wanakwenda tena, Niyonzima anawekwa chini hapa, mpira wa adhabu unapigwa kuelekea lango la Majimaji.

Dk 14, Gooooooooooal! Deus Kaseke anaifungia Yanga bao la kwanza. Niyonzima alipiga krosi kutoka upande wa kushoto, kipa wa Majimaji akaipangua, Kaseke akakutana na mpira na kupiga shuti kali, lililojaa wavuni.

Dk 10, Kaseke anaenda kwa spidi, anakosa kumalizia. Majimaji inatakiwa wawe makini na hawa Yanga maana wanatumia Wings zao (wachezaji wa pembeni).

yanga-7

Dk 7, Msuva anakosa bao tena hapa, namna gani Msuva leo. Yanga wanaonekana kuishambulia kwa kasi Majimaji.

Dk 1, Msuva anakosa bo la wazi hapa hatu chache kutoka langoni na mpira unatoka na kuwa kona kuelekea lango la Majimaji.,

Dk 1, Mpira umekwisha anza, Majimaji wanagusa moja hapa. Mchezo unapigwa katika Uwanja wa Majimaji.

PICHA: MUSA MATEJA/GPL

Comments are closed.