The House of Favourite Newspapers

FT: Yanga 2-0 Tanzania Prisons, Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Taifa, Dar

0

FULL TIME

Dakika ya 94: Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mchezo, Yanga inapata ushindi wa mabao 2-0.

Dakika ya 94: Muda wowote mchezo unaweza kumalizika kuanzia sasa, Yanga wamepunguza kasi kwa kuwa wameshajihakikishia ushindi.

Dakika ya 94: Muda wowote mchezo unaweza kumalizika kuanzia sasa, Yanga wamepunguza kasi kwa kuwa wameshajihakikishia ushindi.

Dakika ya 92: Prisons wanafika langoni mwa Yanga wanapiga shuti linapaa juu ya lango.

Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.

Dakika ya 88: Niyonzima anapiga mpira wa kona lakini kipa wa Prisons anaokoa na inakuwa kona nyingine ambayo ni ya 13 kwa Yanga katika mchezo huu.

Dakika ya 86: Baada ya kufungwa mabao mawili, sasa Prisons wanaanza kuoanda mbele na kupiga pasi kadhaa.

Dakika ya 85: Prisons wanafanya mabadiliko, anatoka Samatta anaingia Kazungu,

 

Dakika ya 75: Yanga wanapata bao la pili kupitia kwa Chirwa ambaye anamalizia pasi nzuri ya kichwa kutoka kwa Tambwe ambaye naye alipata mpira kutoka kwa Haji mwinyi.

 

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!! CHIRWAAAAAAAAAAAA

Dakika ya 73: Yanga wanaendelea ulishambulia lango la Prisons kwa nguvu.

Dakika ya 70: Yanga wanapata bao la kwanza kupitia kwa Amiss Tambwe kwa kichwa, alimalizia kazi nzuri iliyoanza kwa Chirwa kisha Msuva.

Dakika ya 70: GOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!!! Tambweeeeeeeeeeeeeee

Dakika ya 67: Yanga wanalishambulia kwa nguvu lango la Prisons ambao wamerejea nyuma kuzuia.

Dakika ya 66: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Saidi Juma Makapu, anaingia Haruna Niyonzima.

Dakika ya 64: Kassim anagusa mpira wake wa kwanza kwa shuti kali lakini linatoka nje ya lango.

Dakika ya 63: Victor Angaya anatolewa, anaingia Kassim Khamis.

Dakika ya 62: Kelvin Yondani wa Yanga anapata kadi ya njano kutokana na kumchezea vibaya Victor Angaya.

Dakika ya 59: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Kessy, anaingia Juma Abdul.

Dakika ya 58: Kasi ya mchezo imeongezeka kwa timu zote kushambuliana kwa kasi.

Dakika ya 55: Prisons wanafanya shambulizi kali, Meshack Suleiman anaingia kwa kasi akiwa na mpira ndani ya eneo la 18 lakini shuti lake linapaa juu ya lango.

Kipindi cha pili kimeanza.

Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza kwa kipindi cha pili.

MAPUMZIKO

Dakika ya 48: Mwamuzi anapuliza kipenga kukamilisha kipindi cha kwanza, matokeo ni 0-0.

Dakika ya 47: Prisons wanaenda na mpira hadi katikati ya uwanja lakini wanashindwa kujipanga vizuri na wanaupoteza mpira.

Dakika ya 45: Yanga wanafika langoni kwa Prisons wanajigonga wenyewe na mpira unaondolewa. Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 za nyongeza.

Dakika ya 41: Yanga wanapata kona, anapiga Mwashiuiya lakini kipa anadaka.

Dakika ya 40: Bado matokeo ni 0-0, Yanga wanarejea nyuma kujipanga baada ya kufanya mashambulizi mfululizo.

Dakika ya 37: Yanga wanaendelea kulishambulia lango la Prisons, Msuva anapata nafasi ndani ya eneo la 18 lakini anaanguka mwenyewe.

Dakika ya 34: Yanga wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Priosons, Mwashiuiya anapiga shuti kali kipa anapanangua, inakuwa kona.

Dakika ya 32: Yanga wanakosa nafasi ya wazi baada ya Bossou kubaki na lango lakini anapiga shuti linalotoka nje.

Dakika ya 30: Nurdini Chona wa Prisons anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Mwashiuiya, inakuwa faulo, Yanga wanapiga faulo hilo nje ya eneo la 18 la Prisons upande wa kushoto lakini mpira unaondolewa.

Dakika ya 26: Nahodha wa Prisons, Benjamin Asukile anamchezea madhambi Msuva, inakuwa faulo na Benjamin anapata kadi ya njano.

Dakika ya 25: Yanga wanalishambulia lango la Prisons, Msuva anapatga nafasi ya kuingia ndani ya hatari lakini anawahiwa na mpira unaondolewa.

Dakika ya 23: Meshack Selemani anamtoka beki wa Yanga, Hassan Kessy lakini Kelvin Yondani anamuwahi na kumtoa, anamchezea faulo nje ya eneo la 18. Prisons wanapata faulo wanapiga mpira unapaa juu ya lango.

Dakika ya 20: Prisons nao wameanza kucheza kwa kutulia, wanafanya shambulizi la kushtukiza lakini mchezaji wao Angaya anashindwa kumalizia kazi nzuri waliyofanya wenzake.

Dakika ya 15: Yanga wanaonekana kujopanga zaidi huku Prisons wakifanya mashambulizi ya kushtukiza.

Dakika ya 10: Mchezo unaendelea kwa kasi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 5: Simon Msuva anafika kwenye lango la Prisons lakini walinzi wanafanya kazi nzuri ya kuondoa hatari inakuwa kona ambayo imepigwa lakini haikuwa na faida.

Dakika ya 1: Mchezo unaanza kwa kasi kiasi, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika langoni mwa Prisons.

Mwamuzi anapuliza kipenga cha kuanza kwa mchezo huu wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Timu zote zimeungana katikati ya uwanja kisha mwamuzi amepuliza kipenga cha kuashiria kuomboleza kwa dakika moja.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom unaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 56 katika michezo 25, Tanzania Prisons inashika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 31 katika michezo 27.

KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOIVAA TANZANIA PRISONS, LEO PALE TAIFA HIKI HAPA

1. Beno Kakolanya

2. Hassan Kessy

3. Haji Mwinyi

4. Kelvin Yondani

5. Vicent Bossou

6. Juma Said

7. Simoni Msuva

8. Thabani Kamusoko

9. Amisi Tambwe

10. Obrey Chirwa

11. Geofrey Mwashuiya

 

Wachezaji wa akiba:

Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Vicent Andrew, Mateo Antony, Deusi Kaseke , Emmanuel Martin, Haruna Niyonzima.

 

PICHA NA MUSA MATEJA | GPL

Leave A Reply