The House of Favourite Newspapers

Vyakula vya Kukufanya Usizeeke

KIINI CHA YAI

LEO kwenye safu hii nitakuletea vyakula ambavyo ukila vitakufanya usizeeke kwani siku hizi watu wanazeeka haraka licha ya kuwa na umri mdogo. Kama unataka kusafisha ubongo wako ambao huchoka mara kwa mara tumia kiini cha yai, kina wingi wa Klorine ambayo ni virutubisho muhimu vinavyowezesha ubongo kufanya kazi.

COCOA

Kama unafanya urembo wa ngozi hasa chini ya macho kwenye ngozi inayoweka weusi paka cocoa ina wingi wa vitamin itakayosaidia kulinda ngozi yako isizeeke.

KAHAWA NA MAFUTA YA NAZI

Kama unataka kuwa na nguvu kwa siku chukua kahawa yako iweke na vijiko viwili vya chai vya mafuta ya nazi kisha kunywa. Mafuta ya maboga kwa kuondoa msongo wa mawazo

Kama wewe ni mtu mwenye msongo wa mawazo mara kwa mara tumia mafuta ya maboga yana wingi wa asidi ya amino na glutamate ambayo yanasaidia ubongo kukaa sawa na wewe kujisikia vizuri.

Mafuta haya ni mazuri kuyatumia hata kwa mtu mwenye mba kichwani ili kuzitibu yapake kwenye ngozi wakati wa kulala. Kwa ujumla hivi ndivyo vyakula vinavyokufanya usizeeke kama utatumia ipasavyo kwani kila kimoja kina kitu kinachoimarisha kwenye mwili wa binadamu ambacho kama kitakaa vibaya kitakufanya uzeeke.

Comments are closed.