The House of Favourite Newspapers

Waamuzi Jonesia, Zabron, Sudi Wapewa Onyo -Video

0

BODI ya Ligi kupitia Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) imewapa onyo waamuzi wa kati ambao ni Jonesia Rukyaa, Florentina Zabron na mwamuzi wa pembeni, Sudi Lilla, kwa makosa mbalimbali katika mechi tofauti walizochezesha.

 

Kaimu Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayela,  amesema kamati ya Saa 72 iliyokaa jana Januari 29, 2020,  ilipitia taarifa ya Kamati maalum iliyoundwa kupitia matukio mbalimbali ambayo hayakutolewa maamuzi katika michezo miwili Kati ya Yanga na Mbeya City na Simba na Yanga.

 

Amesema mechi Kati ya Mbeya City na Yanga iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya,  Kamati ilipitia matukio ya mechi hiyo na kubaini kuwa Uwanja haukuwa katika hali nzuri kutokana na mvua hivyo kusababisha utelezi, lakini imempa onyo mwamuzi Florentina Zablon na kumtaka awe makini katika utekelezaji wa majukumu yake na kuhakikisha hali ya Uwanja inakidhi matakwa kisheria.

Amesema mwamuzi huyo ameonywa kwa kutumia kanuni ya 39(6) udhibiti wa waamuzi.

Pia Kamati hiyo ilipitia maelezo ya kamati maalum na kubaini kuwa kulikuwa na matukio ambayo hayakuamriwa kwa usahihi na waamuzi Rukyaa na Lilla katika mchezo Kati ya Yanga na Simba uliofanyika Januari 4 mwaka huu, hivyo waamuzi hao wamepewa onyo na kuwataka kuhakikisha kuwa matukio hayo hayajirudii tena.

Mwayela amesema kikao Kingine cha Kamati ya Saa 72 kitafanyika Jumatatu ili kupitia matukio mengine na kuyatolea uamuzi kwa haraka.

Leave A Reply