The House of Favourite Newspapers

Waarabu Wampa Simon Msuva Bil 1.5 Kukiwasha CR Belouizdad Algeria

0
Simon Msuva

IMEELEZWA kwamba, timu ya CR Belouizdad kutoka Algeria, imemtengea winga Mtanzania, Simon Msuva ofa ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 kuinasa saini yake, baada ya nyota huyo hivi sasa kuwa huru.

Msuva ambaye mkataba wake wa kuitumikia Al-Qadsiah FC ya nchini Saudi Arabia ulimalizika Julai 1, 2023, kwa sasa hana timu, huku akiwa amefanikiwa kuzitumikia klabu kadhaa za Ukanda wa Afrika Kaskazini ikiwemo Difaa El Jadida na Wydad Cassablanca.


Chanzo chetu kimeliambia Spoti Xtra kuwa, tayari Msuva ameondoka nchini na kuelekea Algeria kwa ajili ya kujiunga na CR Belouizdad kwa dau hilo la zaidi ya shilingi bilioni 1.5.

“Sasa naweza kukuambia rasmi kuwa, Msuva amepiga chini ofa ya Simba na Yanga, baada ya kupata dili kubwa nchini Algeria, ambapo awali Yanga walimpatia ofa ya shilingi milioni 350 na mshahara wa shilingi milioni 20 kila mwezi.

“Simba wao wakampatia ofa ya shilingi milioni 400 na mshahara wa shilingi milioni 25 kila mwezi ambapo aliwaambia wasubirie atawajibu jambo ambalo limekwama baada ya CR Belouizdad kuingilia dili hilo na kumuhakikishia mshahara wa zaidi ya shilingi milioni 50 kila mwezi, huku wakiweka mezani ofa ya zaidi ya shilingi bilioni moja.

“Tayari Msuva amekwea ndege usiku wa kuamkia leo (jana Jumatano) Agosti 23 tayari kwa ajili ya kwenda kukamilisha dili hilo akiwa sambamba na uongozi unaomsimamia,” kilisema chanzo hicho.

STORI NA MUSA MATEJA

JWTZ WATANGAZA KIAMA – ”SALIMISHENI SARE za JESHI NDANI ya SIKU 7 KWENYE VITUO VYA POLISI”…

Leave A Reply