The House of Favourite Newspapers

Kesi ya Wabunge Waliovuliwa Uanachama CUF Yaanza Kuunguruma Kortini

0
Wabunge hao wakiwa mahakamani.

 

Wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF) waliovuliwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama hicho anayetambulika na Msajili wa Vyama, Prof. Ibrahim Lipumba, leo Agosti 2, 2017 kesi yao imeanza kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

 

Katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo, wabunge hao wameiomba mahakama hiyo kuweka zuio la wabunge wapya kuapishwa hadi kesi ya msingi waliyofungua itakapoamuliwa.

 

Aidha wabunge hao wameiomba mahakama kuzuia utekelezaji wa Uamuzi wa Baraza Kuu la CUF kuwavua uanachama.

Leave A Reply