The House of Favourite Newspapers

Wabunge ‘WAMLIPUA’ Lema, Nassari Mbele ya Rais Magufuli – Video

Rais Dkt John Magufuli, leo Disemba 02, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wilayani Arumeru mkoani Arusha. Hafla ya uzinduzi huo imehudhuriwa na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa, Katibu mkuu wa wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo, Aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo ambaye kwa sasa ni Waziri wa Ujenzi, Dkt Isaac Kamwelwe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na Wakuu wa wilaya za Arusha akiwemo, Jerry Muro, ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Arumeru mahali ambapo mradi huo unazinduliwa. Kabla ya hotuba ya Rais Magufuli, baadhi ya Wabunge wanaouwakilisha mkoa wa Arusha, akiwemo Catherine Magige, Amina Mollel, wakapata fursa ya kutoa salamu zao mbele yake na kisha kuziwasilisha shida za wananchi wa mkoa huo.

Comments are closed.