The House of Favourite Newspapers

Wabunge wapongeza uwekezaji unaofanywa na SBL

0
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Mark Ocitti, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo jijini Dar es Salaam

Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge wamepongeza uwekezaji unaofanywa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL)unaohusisha upanuzi wa kiwanda chakecha Dar es Salaam. Kampuni ya SBL inafanya upanuzi wa kiwanda cha Dar es Salaam, moja kati ya viwanda vyake vitatu. Upanuzi huo unaogharimu Paundiza Uingereza milioni 10, utasaidia kuongeza uzalishaji wa bia ilikukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wateja wa kampuni hiyo.

Akiongea muda mfupi baada ya kutembelea kiwanda cha Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo Mahimba Ndaki alisema,uwekezaji huo utasaidia kutatengeneza ajira mpya kwa Watanzania na kuongeza mahitaji ya malighafi za kuzalisha bia kama shayiri, mahindi na mtama jambo ambalo litawaongezea wakulima kipato.“Uwekezaji wenu endelevu unaenda sambamba na agenda  yetu ya Tanzania ya viwanda.

Uwekezaji mkubwa kama huu unatia moyo na unaonyesha namna ambavyo mmejipanga vyema kutumia fursa zilizopo katika Tanzania ya Viwanda. Sisi tuna wahakikishia ushirikiano wetu katika shughuli zenu za kila siku,” alisema Ndaki.

Mkurugenzi wa Mahusiano kwa Umma wa SBL  John Wanyancha aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kwamba, upanuzi wa kiwanda hicho upo katika hatua za mwisho za kukamilika na kuongeza kuwa utasaidia kuongeza ajira pamoja na mapato kwa Serikali kupitia kodi.

Meneja operesheni wa kampuni ya SICPA inayoendesha mfumo wa stempu za kielektroniki viwandani, Ibrahim Marwa (wa kwanza kushoto), akiwaelekeza jambo wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Bunge waliotembelea kiwanda cha bia cha Serengeti

Wanyancha  aliongeza kuwa, kwasasa SBL inanunua Shayiri,    mahindi pamoja na mtama kutoka kwa wakulima wazawa kwaajili ya uzalishaji wa bia zake nakwamba mwaka jana ilinunua tani za ujazo 17,000 sawa na asilimia 70 yamahitaji yote  ya malighafi ambayo SBL inatumia kwa mwaka

SBL imeajiri zaidi ya wafanya kazi 700 moja kwa moja na wengine maelfu kwa ajira zisizo za moja kwa moja kupitia mlolongo  wa thamani ya biashara zake katika viwanda vyake vya Dar es Salaam, Moshi na Mwanza.

 

Leave A Reply