The House of Favourite Newspapers

Wachezaji 11 nje Yanga SC

0

YANGA (2)Wachezaji wa timu ya Yanga.

Sweetbert Lukonge
na Nicodemus Jonas
BALAA kubwa limeikumba Yanga ambayo hivi sasa ipo katika maandalizi makali ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza wikendi ijayo baada ya wachezaji wake kushindwa kufanya mazoezi.

Timu hiyo ambayo kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 39, imekumbwa na balaa la nyota wake 11 wa kutumainiwa kuwa nje ya uwanja wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Hali hiyo imeonekana kuwachanganya vilivyo viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm.

YANGA (1)Wachezaji hao ni Amissi Tambwe, Simon Msuva, Malimi Busungu, Vincent Bossou, Boubacar Garba, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Deogratius Munishi ‘Dida’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na Juma Abdul.
Licha ya baadhi yao kufika mazoezini jana asubuhi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani, Ununio lakini hawakujumuika na wenzao.

YANGA (3)
Katika orodha hiyo, Busungu, Tambwe, Mwinyi, Cannavaro, Garba wao hawakufika kabisa.
Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya, aliambia gazeti hili kuwa, wote wana matatizo tofauti na kwamba anajitahidi kadiri ya uwezo wake kuhakikisha wanarejea kikosini mara moja.
“Ni kweli wachezaji hao hawapo vizuri kiafya lakini tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha wanakuwa sawa.
“Hata hivyo, Twite, Juma, Bossou na Msuva kesho (leo), wanaweza kuungana na wenzao mazoezini, hao wengine waliobaki kama mambo yatakwenda vizuri basi watarejea uwanjani baada ya muda mfupi,” alisema Matuzya.

Leave A Reply