The House of Favourite Newspapers

Mabao 13 Yanga yampa Tambwe hofu

0

AmissTambwe2Straika wa Yanga na kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Amissi Tambwe.

Khadija Mngwai,
Dar es Salaam
STRAIKA wa Yanga na kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, Amissi Tambwe, amesema bado ana safari ndefu kuhakikisha anafanikiwa kutwaa kiatu cha dhahabu mwishoni mwa msimu kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

Tambwe amefanikiwa kufunga mabao 13 hadi sasa na kuwa kinara wa mabao huku akimuacha mbali Hamisi Kiiza wa Simba mwenye mabao kumi, Donald Ngoma wa Yanga na Elias Maguri wa Stand United wote wakiwa na mabao tisa kila mmoja.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe raia wa Burundi amefunguka kuwa, anafurahi kuona anaongoza katika ufungaji lakini bado ana kibarua kikubwa mbele kutokana na ushindani uliopo, hivyo anahitaji kujituma zaidi ili kufikia malengo.
“Siku zote napenda kuwa juu ya wengine kuona ninafanikiwa, nimefurahi kuona nina mabao 13 lakini bado nina changamoto kubwa ya kuweza kujituma ili kufanikiwa kukitwaa kiatu hicho.
“Ushindani bado upo mkubwa sana kutokana na kila mchezaji kuhitaji kufanikiwa kuibuka mshindi hivyo kama sitajituma naweza kushindwa kutimiza malengo yangu, mabao niliyonayo siyo mengi sana natakiwa kufunga zaidi,” alisema Tambwe ambaye alikuwa mfungaji bora msimu wa 2013/14.

Leave A Reply