The House of Favourite Newspapers

WACHEZAJI 20 WA YANGA KUIVAA ST. LOUIS JUMATANO

Kikosi cha timu ya Yanga SC.

KIKOSI cha Yanga Sc kinatarajia kusafiri kesho asubuhi kueleka Shelisheli tayari wa mchezo wa marejeano na wenyeji St Louis Fc kwenye ligi ya mabingwa afrika mchezo ulipangwa kuchezwa jumatano ijayo Stade Liete.

Muda mfupi  uliopita  Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten ameiambia  yangasc.co.tz kuwa  jumla ya nyota 20 na viongozi 10 kati yao 8 kutoka benchi la ufundi watasafiri asubuhi ya kesho  kupitia Nairobi tayari kwa mchezo huo muhimu  siku ya jumatano.

“Maandalizi yote muhimu yamekwisha fanyika, timu imefanya mazoezi ya mwisho leo tayari kwa safari hiyo, kwenye kikosi nyota waliokuwa na majeraha ya muda mrefu kama Amissi Tambwe, Donald Ngoma, Abdallah Shaibu na Yohana  Mkomola wataendelea  kukosekana hii ni kwa sababu bado wanauguza majeraha, kucheza ugenini kuna changamoto zake lakini tumejiandaa vizuri kwa sababu tushacheza nje mara nyingi hivyo hakuna hofu kati yetu.”

Akiendelea zaidi Ten alisema kuwa, mchezaji Thabani Kamusoko ambaye amepona majeraha yake hivi karibuni na kuanza mazoezi mepesi pia ameondolewa kutoka orodha ya nyota ambao wangesafiri kueleka Shelisheli ili apate muda wa kujifua zaidi ili kurejesha makali yake, mchezaji Obrey Chirwa  naye hayumo kwenye orodha ya wachezaji watakaosafiri kwa sababu ya maumivu ya misuli aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Majiamaji.

“Ilikuwa asafiri  kueleka Shelisheli, lakini imelazimu benchi la ufundi kumuondoa kwa sababu bado hajawa ‘fit’ asilimia 100,anahitaji muda wa kujifua zaidi ili kupata utimamu wa mwili tayari kwa mapambano uwanjani,daktari wake pia amethibitisha kuwa mchezaji anatakiwa apate muda wa kujiweka sawa kabla hajaanza kucheza mechi kulingana na majeraha aliyokuwa nayo.”

Orodha kamili ya wachezaji ambao safiri kuelekea Shelishelini kama Ifuatavyo:

Ramadhani Kabwili, Beno Kakolanya, Youthe Rostand, Hassan Kessy, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Gadiel Michael, Nadir Haroub, Patto Ngonyani, Kelvin Yondani, Said Juma, Papy Tshishimbi, Pius Buswita,Raphael Daud, Yussuf Mhilu, Ibrahim Ajib,S aid Mussa, Emmanuel Martin, Geoffrey Mwashiuya, Juma Mahadhi.

Comments are closed.