The House of Favourite Newspapers

Wadau wa Sekta ya Utalii Wajadili Jinsi ya Kukuza Sekta Hiyo, Dar

0

1.Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.2.Wadau waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini maada zilizokuwa zikijadiliwa.Wadau wakifuatilia kwa makini maada zilizokuwa zikijadiliwa.3.Mkutano ukiendelea.Mkutano ukiendelea.4.Katibu Mkuuu wa Wizara ya Mali asili na Utalii, Dk.Adelhelm Meru akizungumza jambo kwenye mkutano huo.Katibu Mkuuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Adelhelm Meru akizungumza jambo kwenye mkutano huo.5.Dk.Meru akitoa mapendekezo yake yaliyokuwa yakihusu namna ya kukuza sekta ya ukarimu na  utalii.Dk. Meru akitoa mapendekezo yake yaliyokuwa juu ya namna ya kukuza sekta ya ukarimu na utalii.6....mkutano ukiendelea ukumbini hapo.…mkutano ukiendelea ukumbini hapo.7.

Wadau wa sekta ya utalii wakiendelea kufuatilia mkutano huo.

9.Dr. Adelhelm Meru akihojiwa na wanahabari mara baada ya kumalizika mkutano huo.Dr. Adelhelm Meru akihojiwa na wanahabari mara baada ya kumalizika mkutano huo.

WADAU wa sekta ya utalii na wawekezaji hapa nchini, wamekutana hii leo kujadili namna ya kukuza sekta ya ukarimu na utalii wakiwa na lengo la kuendeleza na kukuza dira ya pamoja ya maendeleo na harakati za kati na wadau wa sekta binafsi na sekta ya umma.

Mkutano huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jengo la Mwalimu Nyerere International Convention Centre (JINCC) jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kufikia kikomo kesho Jumanne.

Mkutano huo umeandaliwa na Internationala Hospitality Consultancy HD Partnership kwa kushirikiana na shirika la wamiliki wa Hotel Tanzania (HAT) ikiwa ni mkutano wa pili kufanyika hapa nchini kuzungumzia malengo yanayohusu ukarimu na utalii katika nchi zilizopo Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa katika mkutanao huo ni juu ya ukarimu wa wadau wa sekta za utalii wakiwemo wawekezaji, wamiliki wa hoteli, kampuni za usimamizi bidhaa, mashirika ya kiserikali, wasambazaji na watoa huduma kwenye hoteli za kitalii na namna ya kuchochea ukuaji endelevu wa sekta hizo kwa kutoa wataalam, kutoa ushauri ikiwemo kutengeneza mazingira ya maonyesho ambayo yatatoa fursa za kubadilishana ujuzi baina ya makampuni mbalimbali.

Akizungumza kwenye mkutano huo, mmoja wa washauri wa kimataifa na ukarimu wa masuala ya utalii, Meelis Kuuskler, amesema kuwa mkutano wa mwaka huu umejikita katika masuala maalum ya kiutendaji yanayoathiri shughuli za utalii na jinsi ya kuinua ubora wa rasilimali watu na kuchochea zaidi mazingira mazuri ya biashara kwa maendeleo mapya.

Amesema kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na jukwaa la uchumi duniani, Tanzania inashika nafasi ya saba kati ya nchi 141 kwa mwaka 2015 katika ushindani wa sekta ya utalii kutokana na rasilimali zilizopo za asili kuwa nyingi.

Aidha kwa upande wa wajumbe waliohudhuria mkutano huo walitoa mapendekezo yao kwa kusema kuwa uwezo wa sekta binafsi katika kutekeleza mabadiliko ya uchochezi katika utalii utakuwa bora kama utalindwa na ushirikishwaji wa wazi kupitia sekta za umma.

Na DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply