The House of Favourite Newspapers

Wadau Waombwa Kuisapoti Timu ya ‘Wheelchair Tennis’

0

WADAU mbalimbali wa mchezo wa tennis inayochezwa kwa kutumia baiskeli za miguuu mitatu (Wheelchair) nchini wameombwa kuchangia timu hiyo ambayo inatarajia kwenda kushiriki michuano ya dunia ya mchezo huo nchini Italia kufuatia timu hiyo kufuzu na kuibuka kidedea na kuwa mabingwa wa mchezo barani Afrika.

Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu (kulia) akizungumza na wanahabari.

Kituo cha televisheni cha TV1 nchini kwa kushirikiana na chama cha Tennis Tanzania imezindua mchakato maalum wa kuchangia timu ya taifa  ya Wheelchair (Paralympics).

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa TV1, Gillian Rugumamu,  alisema: “Tumepata  wito wa kushirikiana na ndugu zetu baada ya kuguswa na stori ya vijana hawa wa Wheelchair Tennis Tanzania.   Vijana hawa wamekuwa ni mabingwa wa mchezo huu barani Afrika na kupata tiketi ya kushiriki katika michuano ya dunia.

Mwakilishi wa wadhamini wa mashindano hayo, Namiundu Ngutupari ‘Jeshi’ (katikati) kutoka Times Fm akifafanua jambo.

“Wamekuwa wakiwakilisha nchi yetu Tanzania vizuri katika michuano mbalimbali na kushinda bila watu wengine kutambua hilo, hivyo sisi tumekuwa wadau wakubwa wa michezo mbalimbali hususani katika kipindi hiki ambacho kituo chetu cha televisheni kimezindua michezo mbalimbali ikiwepo, EPL, NBA, Formula 1na michezo mingine.’’

Naye mwakilishi kutoka chma cha Tennis Tanzania, Dennis Makoi, alisema kwamba chama kwa kupitia makocha kimendelea kuwatafuta wachezaji na kuwafundisha katika sehemu mbalimbali, mashuleni,  mitaani na sehemu nyingine tofauti jambo ambalo  limetokana na mwamko walioupata baada ya kushinda medali na tuzo katika nchi mbalimbali ikiwemo Uturuki.

Katibu Mkuu wa Chama cha Tennis, Irene Jackson (Kulia) akifafanua jambo.

“Katika kufanikisha safari hii timu inahitaji tiketi 10 za ndege, fedha za malazi na chakula, vifaa vya michezo kama vile Wheelchair (baiskeli) tennis rackets, viatu vya kuchezea, madawa na bima ambapo jumla yake ni milioni 120,000,” alisema.

Leave A Reply