The House of Favourite Newspapers

Niyonzima Ambakisha Omog Simba

0
Haruna Niyonzima.

KIUNGO mchezeshaji wa Simba, Haruna Niyonzima, ametamka kuwa kati ya vitu ambavyo watavikosea katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara, basi ni kumuondoa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mcameroon, Joseph Omog.

 

Timu hiyo, hivi karibuni ilidaiwa kuwepo kwenye mipango ya kumuondoa Mcameroon huyo ambaye amecheza michezo mitano ya ligi, kati ya hiyo ameshinda mitatu na ametoa sare miwili.

 

Kati ya makocha waliokuwa wanatajwa kuja kuchukua nafasi ni Mserbia, Goran Kopunovic aliyewahi kuifundisha timu hiyo.

 

Akizungumza na Global TV Online, Niyonzima alisema ni ngumu kutathmini uwezo au kiwango cha ufundishaji cha Omog kwenye mechi tano ambazo wamezicheza katika ligi kuu.

 

“Niwe mkweli, ni mapema kutathmini uwezo wa kocha Omog, ninaamini ni kocha mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kufundisha na timu kupata matokeo mazuri.

 

“Changamoto anayokabiliana nayo Omog ni ujio wa wachezaji wapya zaidi ya kumi ambao wamesajiliwa kwenye msimu huu wa ligi kuu nikiwemo mimi,” alisema Niyonzima.

Kushuhudia mahojiano kamili, tembelea akaunti ya Global TV Online kwenye mtandao wa YouTube

Leave A Reply